Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japo majanga mengine hayaepukiki tahadhari ni muhimu:UNEP

Kimbunga Idai kimesababisha uharibifu kwa asimia 90 katika jiji la Beira.
WFP/Andrew Chimedza
Kimbunga Idai kimesababisha uharibifu kwa asimia 90 katika jiji la Beira.

Japo majanga mengine hayaepukiki tahadhari ni muhimu:UNEP

Tabianchi na mazingira

Hivi karibuni katika maeneo mengi ya Afrika Mashariki hali ya joto la kupindukia, mafuriko na kuchelewa au kukosekana kwa mvua imekuwa ni gumzo kubwa huku wakulima wakihaha kuokoa mazao yao.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira vyote hivi ni dalili dhahiri ya mabadiliko ya tabianchi na hivyo kuzitaka nchi kuchukua hatua stahili ili kuhimili na pua kuwanusuru wananchi wake pindi majanga ya asili yanapozuka. Ili kufahamu zaidi kuhusu mabadiliko haya ya tabia nchi yanayoeleta zahma kubwa ikiwemo ukame , mafuriko na hata vimbunga kama IDAI mwandishi wetu Stella Vuzo wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam Tanzania amezungumza na Bi Clara Makenya mratibu na afisa wa UNEP nchini humo

MAHOJIANO YA STELLA VUZO NA CLARA MAKENYA

Clara Makenya

Ukiangalia hivi sasa tukiongea kuhusiana na suala la  kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi  hatuangalii tu kupanda miti au fanya hivi, tunangalia upande mkubwa  zaidi wa kukabiliana kama wanadamu. Kwanza naweza nikasema mfumo wa majengo, ndio maana, Stella mabadiliko ya tabianchi sasa hivi sio suala tu la wanasayansi  wa kundi fulani , ni kila mtu. Ni wajenzi, ni wakulima ni wafanyabiashara, kwa mfano sasa kuhusu hii IDAI ilikuwa ni Cyclone kubwa  sana na imeleta  athari kubwa sana  lakini unaweza kusema kwamba labda yale maeneo yaliojidhatiti zaidi labda inawezekana  ,hatari zake hazikuwa  kubwa kama kwingine. Sana sana katika mfumo wa ujenzi, na hicho ndio kitu ambacho tunahamasishwa sasa hivi kwa habari ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kuepuka hayo maafa kama hivyo. Tunavyoendelea kuangalia jitihada muda murefu , kwamba tupande miti, tuangalie mfumo mzima wa maisha uko namna gani , tusizidi kuongeza zile sababisho za  mabadiliko ya tabianchi na kadhalika. Tunavyokuwa tunaangalia pia tuagalie kwajinsi gani tunakabiliana na hii inapotokea, kwa mfano kama hivi naweza nikatoa mfano  labda wa huu mradi tulioufanya hapa Ocean road sisi hapa Tanzania . Tulitengeneza , tuseme tumehimarisha na kujenga ukuta wa bahari. Vitu kama hivyo, kukabiliana na vitu ambavyo  sasa hatuna uwezao navyo. Kwasababu sasa kama hiyo Cyclone imejitengeneza na inatokea. Mifumo yetu ya ujenzi iko namna gani? Je ipo katika hali ya kuweza kukabiliana na Cyclone? Lakini mwisho wa hapo pia hata hii Cyclone inavyoteokea imeathiri sana , kwanza watu wamepoteza  maisha yao, lakini itakuwa kwa kiasi kikubwa imeathiri uchumi kwa kiasi kikubwa sana. Ni jinsi gani watu wanakabiliana na hali ya uchumi ambao umekuwa imeathiriwa na hii Cyclone kwa mfano. Kwa hiyo kwenye kona zotezote tunapaswa macho yetu yaangalie kwa mtazamo mkubwa zaidi. Kuna watu wamepoteza maisha, uchumi umeathiriwa, miundombinu imeathiriwa ina maana maeneo yote hayo katika mpangilio wa maendeleo wa nchi yanatakiwa kuangaliwa. Labda kwa mfano kitu kama hicho kimetokea Tanzania, je tumejipanga vizuri? Miundombinu yetu iko vipi? Je wananchi wetu wamefundishwa au wameelekezwa jinsi gani wanaweza kukabiliana na mazingira kama haya?

Stela Vuzo

Kwa hiyo kwa mfano  unasema wanainchi wetu wanafundishwa, wewe mwenyewe kama mtaalamu unapendekeza nini kifanyike sasa kwenye mataifa kwajili ya kuchukua taadhari au kijikinga dhidi ya matatizo kama haya?

Clara Makenya

Bahati mbaya sana  kuhusiana na hizi hatari ambazo ni za asilia, kuna kiwango fulani mwanadamu anaweza akafika, cha kuzuilia hatari zisifike kiasi kilichotokea lakini kuna kiwango ambacho yaani ni Mungu tu aingilie kati . Nasema hivyo kwa ujasiri kwasababu naweza niakatolea mfani wa Japan, unakumbuka  kipindi cha Sunami Japan na miundumbinu yake ilivyokuwa misuri, lakini utakuwa umeona kwenye video jinsi magari yalisukumwa, nyumba zilisukumwa sasa  nchi kama Japan na kuendelea kwake. Kwa hiyo nataka kusema kwamba kuna kiwango ambacho unaweza kukifanyia kazi wewe kama mwanadamu. Ndio maana inaturudishia huko nyumba kusema kwamba twende sambamba kuzuilia hatari za namna hiyo zisitokee, lakini kwangalia pia ni jinsi gani tunaweza tukakabilina na hatari kama hizi punde zinapotokea. Sasa kimoja wapo kwa mfano kukabiliana na hatari hizi zisitokee au zisiwe na ukubwa ambao unakuja kwa kadri tunavyoweza , ni kwenye eneo la miundombinu  ni kwenye eneo la kuendeleza na kuelelimisha mifumo ya kusoma labda hali ya hewa kwa mfano (Tanzania Meterological agency) kusaidia kuwezesha kusoma kwa uhalisia  hali ya  hewa , wanaweza wanakatoa taadhari kwa wananchi  ya kwamba hapa jamaani tarehe fulani kuna Cyclone, ikiwezekana wanachi hameni , unaona! Kwa hiyo wananchi  wanahama kwasababu hiyo ni kutu ambayo hawana jinsi ya kuendelea kupambana nayo, unanielewa, kwa hiyo ndivyo wanavyofanya wenzetu wengi hata kule Marekani , unaona wanahamisha watu . Watu wanapohama kweli huku nyuma yanatokea kwa hiyo maafa yanakuwa hayatokei kwa kiasi kile. Lakini upande mwingine pia , nikujidhatiti pie kwenye kuangalia miundombinu ambayo imewekwa hapo. Kama Japan iliweza kusukumwa na magari yake na madaraje yake yakabomolewa katika kiwango cha uwezo wa  miundombinu ya  Japan, unaweza ukaona kweli kuna kiwango ambacho mwisho wa siku ni sisi kuona ni jinsi gani tunaepusha maafa kama hiyo kutoa taarifa mapema zilizo sahihi ili watu kuweza kuondolewa mapema kabla maafa kama haya.