Hata kama wana matatizo ya kujifunza , elimu ni haki yao- Michael Okiro

21 Machi 2019

Leo ni siku ya ugonjwa unaoathiri uwezo wa kujifunza duniani au Down syndrome, ukiwa umebeba kaulimbiu   “kutomuacha mtu yeyote  nyuma kielimu” suala ambalo ni  changamoto kubwa kwa nchi nyingi. Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la afya duniani hatua zimeanza kuchukuliwa na baadhi ya mataifa kutimiza lengo la kuhakikisha watoto wanaozaliwa na matatizo uwezo wa kujifunza wanapata elimu. Uganda ni miongoni mwa nchini zilizopiga hatua kwa kuweka sharia za kuhakikisha   elimu inatolewa bure kwa watu wenye ugonjwa huu.

Akizungumza  na idhaa ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya simu kutoka Kampala Uganda , Mkurugenzi wa taasisi ya Uganda ya watoto wanaozaliwa wakiwa na down Syndrome Dkt Michael Okiro Obwokor anafafanua kinachofanywa na serikali kuhakikisha hilo

(Sauti Ya Dkt Michael Okiro Obwokor)

Na kuhusu wajibu au jukumu la  jamii na wazazi kuhakikisha watoto hao  wanahamasishwa  amesema ….

(Sauti Ya Dkt Michael Okiro Obwokor)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter