UN yataka watu wenye ugonjwa unaoathiri ujifunzaji, kushirikishwa zaidi.  

21 Machi 2021

Ikiwa leo ni siku ya ugonjwa unaoathiri uwezo wa kujifunza duniani au Down syndrome, Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuwashirikisha zaidi watu wenye changamoto hiyo hususani wakati huu wa janga la virusi vya corona.

 Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kila mwaka wastani wa watoto 3 hadi 5,000 huzaliwa na ugonjwa huo. 

Watu walio na tatizo hilo la ujifunzaji wako katika maeneo  yote ya ulimwengu. Kiujumla ugonjwa huo una athari tofauti kwa mitindo ya kujifunza, tabia ya mwili na afya. 

Kaulimbiu yam waka huu ni ujumuishaji na ushiriki.  

Umoja wa Mataifa unaona inawezekana kuwajumuisha watu wenye tatizo la ujifunzaji kwa usawa katika ushiriki wao katika jamii. 

Wataalam wanasema inawezekana kufikia mabadiliko chanya ambayo yanasababisha huduma sahihi ya afya, mipango ya utatuzi na hatua pamoja na ujumuishaji kwa ajili ya Watoto wenye tatizo hilo la Down syndrome.  

 “Ubora wa maisha wa wale ambao wana tatizo la ujifunzaji unaweza kuboreshwa na huduma ya afya kulingana na mahitaji ya kila mtu, pamoja na uchunguzi wa mara kwa mara na ufuatiliaji wa akili na mwili.” Unasema Umoja wa Mataifa.  

Siku hii ya ilipitishwa na Umoja wa Mataifa mnamo 2011, na inatumiwa kuhamasisha sekta mbali mbali za jamii kukuza ujumuishaji na ushiriki sawa wa watu wenye ugonjwa huo ulimwenguni. 

 

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter