Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamlaka Zanzibar wapongeza programu ya kujitolea ya UN

Wafanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Matairfa na wanachama wa mashirika mashinani wakifanya usafi Goma nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC
UN Photo/Sylvain Liechti
Wafanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Matairfa na wanachama wa mashirika mashinani wakifanya usafi Goma nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC

Mamlaka Zanzibar wapongeza programu ya kujitolea ya UN

Masuala ya UM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameipongeza azma ya Umoja wa Mataifa (UN) kupitia programu yake ya kujitolea ya Umoja huo (UNV) kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika shughuli za maendeleo.

Dk. Shein ameyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Mratibu Mkuu wa Programu ya Kujitolea ya Umoja wa Mataifa (UNV) Oliver Adam, aliyefika Zanzibar kwa lengo la kuimarisha mashirikiano baina ya pande mbili hizo.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Mratibu huyo kuwa (UNV) ni programu muhimu iliyo chini ya Umoja wa Mataifa ambayo ina umuhimu mkubwa katika kuendeleza shughuli mbali mbali za maendeleo hapa Zanzibar.

Alieleza kuwa progmu hiyo ya Umoja wa Mataifa imeanza miaka mingi na kuwez kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza na kuunga mkono juhudi za serikali katika shughuli za maendeleo ikiwemo sekta ya afya, kilimo na sekta nyenginezo.

Naye Mratibu Mkuu wa Programu ya Kujitolea ya Umoja wa Mataifa (UNV) Oliver Adam alimueleza Rais Dk. Shein azma ya Progmau hiyo katika kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Zanzibar nayo itafaidika.