Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujitolea kunaimarisha mshikamano na ujumuishi- Naoual Driouich

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kujitolea, Naoual Driouich akizungumza na UN News kabla ya maadhimisho ya siku ya kujitolea ya mwaka 2019
UN News/Elizabeth Scaffidi
Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kujitolea, Naoual Driouich akizungumza na UN News kabla ya maadhimisho ya siku ya kujitolea ya mwaka 2019

Kujitolea kunaimarisha mshikamano na ujumuishi- Naoual Driouich

Masuala ya UM

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kujitolea, Mkuu wa Mifumo ya Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya wanaojitolea ya mjini New York Marekani, UNV, Naoual Driouich katika mahojiano na UN News amesema kujitolea hufungua milango na huleta amani na maendeleo katika jamii zote, kitaifa na kimataifa.

Bi Driouich anaanza kwa kueleza kuwa katika mfumo wa Umoja wa Mataifa ambao una mashirika mengi yanayoshughulikia maisha ya watu kwa namna mbalimbali, kila mwaka kuna watu takribani elfu sita na mia tano ambao wanajitolea kujumuisha na zaidi vijana elfu mbili wanaochangia katika uwasilishaji bora wa amani na maendeleo vinavyofanywa na Umoja wa Mataifa na ambapo kwa mwaka huu wamefikiaa watu elfu nane wanaojitolea kote duniani katika mifumo ya Umoja wa Mataifa.

Naoual Driouich akizungumzia maadhimisho yam waka huu ya siku ya kujitolea ameongeza akisema, “lengo la Siku ya kimataifa ya kujitolea mwaka huu siyo tu kuadhimisha kujitolea na mambo yake yote bali pia kusisitiza  jukumu  la  ujitoleaji na wanaojitolea  katika kuimarisha  mshikamano na  ujumuishi.”

Aidha Bi Driouich amesema, “kujitolea kunatoa fursa kwa watu, hususani wale ambao mara nyingi wametengwa katika kuweza kushirikia katika kuboresha maisha yao na jukumu la kushiriki katika jamii zao kwa kujitolea muda wao na stadi zao.  Kupitia kujitolea,  jamii kote duniani mara nyingi inapata  ushirikiano na ujumuishi na ndiyo maana maadhimisho ya mwaka huu tumechagua kauli mbiu ya ujitolaji kwa  mstakabali jumuishi ili kusisitiza lengo namba 10 la maendeleo endelevu.”

Bi Driouich anamaliza kwa kuwatakia sikukuu njema watu wote wanaojitolea kote duniani, “ningependa kuwatakia siku njema watu wote wanaojitolea na pia kuwashukiuru kwa kazi yao ya na mchango wao wa  kuhamasasisha amani na maendeleo  na pia kwa kutomwacha yeyote nyuma. Kwa hivyo kheri ya sikukuu ya kujitolea”