Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pongezi wanawake Somalia kwa juhudi na ujasiri:UNSOS

Mbunge katika bunge la Somalia, akipiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais mwaka 2017. Katika mabadiliko ya katiba uchaguzi ujao utakuwa mtu mmoja kura moja.
UN Photo/Ilyas Ahmed)
Mbunge katika bunge la Somalia, akipiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais mwaka 2017. Katika mabadiliko ya katiba uchaguzi ujao utakuwa mtu mmoja kura moja.

Pongezi wanawake Somalia kwa juhudi na ujasiri:UNSOS

Wanawake

Jopo la mawasiliano la Umoja wa Mataifa nchini Somalia linaadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kuwapongeza wanawake wa Somalia kwa mchango wao mkubwa katika ujenzi wa amani, maridhiano na kuchagiza usawa wa kijinsia nchini humo.

Kwa mujibu wa jopo hilo siku ya wanawake duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Machi 8, kwa mara ya kwanza iliadhimishwa mwaka 1975 ni wakati wa kutafakari hatua zilizopigwa katika kuelekea haki kamili za wanawake na pia kusherehekea na kuenzi vitendo vingi ya kijasiri na dhamira vinavyofanywa na wanawake kutoka kila nyaja ya Maisha ambao wamekuwa na jukumu kubwa katika historia ya wanawake kwenye nchi na jamii zao. Kaulimbiu yam waka huu ni “fikra sawa, ujenzi yakinifu na ubunifu kwa ajili ya mabadiliko.”

Maadhimisho haya ya siku ya wanawake Somalia yamekuja wakati muafaka na muhimu wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mtu mmoja -kura moja hapo 2020 uchaguzi ambao unaahidi kuwapa kauli kubwa wanawake wa Somalia kuhusu uendeshaji wa kisiasa wa taifa lao na jinsi rasilimali za nchi hiyo zinavyotumika.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa wanawake nchi Somalia wamepiga hatua kubwa katika ukumbi wa masuala ya umma na kisisasa ikiwemo ongezeko la asilimia 10 (kutoka asilimia 14-24) kwenye uwakilishi wa wawanawake kkatika bunge tangu mwaka 2016.

Imeongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa ambalo likiungana linaweza kuleta athari chanya katika jamii ya kisomali.

Mkuu wa ofisi ya umoja wa Mataifa ya usaidizi Somalia , UNSOS Lisa Filipetto amesema “Kama wanawake kwenye jamii zetu na kama mfanyakazi wa UN sote tunajaribu kujenga dunia yenye usawa na uwiano ambayo inawakilisha Nyanja mbalimbali , mahitaji na malengo.”

Ameongeza kuwa katika siku ya wanawake duniani “Nawachagiza nyote kuleta fikra zenu, akili, , uzowefu na ubunifu katika mtihani huu. Lakini nawashukuru hususan wanawake wafanyakazi wenzangu kwa ajili ya kujitoa kwao kusongesha mbele mpango wa malengo ya Umoja wa Mataifa na maadili yake, pia kwa moyo wangu wote nawapongeza wanawake wa Somalia kwa juhudi zao za amani na ujenzi wa taifa.”

Jopo la Umoja wa Mataifa la mawasiliano nchini Somalia linajumuisha maafisa habari wanaohusiana na UNSOS, mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM, mashirika ya Umoja wa Mataifa , operesheni zinazoendeshwa na Umoja wa Mataifa nchini humo.