Masuala ya siasa, uchumi , na usalama kutamalaki juwaa la ubia na Somalia

16 Julai 2018

Jukwaa la ushirika na Somalia  limeanza leo mjini  Brussels Ubelgiji kujadili mambo matatu muhimu ambayo ni siasa, uchumi na usalama.

 Katika jukwaa hilo la, siku tatu, serikali ya Somalia pamoja na washirika wake wanaangazia njia zitakazosaidia kudumisha amani na maendeleo katika taifa hilo la pembe ya Afrika. Lisa Filipetto ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosaidia Somalia, UNSOS, ambae anahudhuria mkutano huo. kabla ya kuelekea Ubelgiji  kwenye jukwaa hilo ameiambia  UN News  kuhusu madhumumi kuwepo kwa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.

 (SAUTI YA LISA FILIPETTO)

“ Kuwepo kwa Umoja wa Mataifa nchini Somalia kuna nia ya kuisadia taifa hilo katika juhudi zake za  kuleta amani na utulivu nchini humo  ambazo zimegawanyika katika mafungu matatu: siasa, maendeleo ya kiuchumi suala la usalama.”

Ofisi ya UNSOS inasaidia  askari 21,000 wa Muungano wa Afrika wa kulinda amani nchini Somalia-AMISOM, wakishirikiana na wanajeshi na polisi wa taifa hilo. Bi Filipetto amesema serikali ya Somalia inajitahidi.

(SAUTI YA LISA FILIPETTO)

“ Lazima tukubali juhudi za serikali ya shirikisho la Somalia kwa kupambana uso kwa uso na changamoto wanazokabiliana nazo katika sekta mbalimbali kwani kisiasia wamepiga hatua kuhusu mfumo wa shirikisho wakilenga uchaguzi mkuu wa 2020,  na wanaifufua katiba yao nadhani hilo ni suala muhimu.”

Baadhi ya washirika katika jukwaa hilo la ubia na Somalia ni Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, na  Muungano wa Afrika.

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter