Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa bado kuna changamoto , matumaini pia yapo katika kulinda mazingira:UNEP

Taka zilizokusanywa ufukweni Bali
UNEP/Shawn Heinrichs
Taka zilizokusanywa ufukweni Bali

Ingawa bado kuna changamoto , matumaini pia yapo katika kulinda mazingira:UNEP

Tabianchi na mazingira

Changamoto za mazingira kuanzia uchafuzi wa hali ya hewa hadi matumizi ya plastiki na athari zake kwa viumbe vya bahari bado ni kubwa lakini kuna matumaini ya kukabiliana nazo imesema ripotri ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingiza , UNEP.

Ingawa safari bado ni ndefu katika kuvishinda vita hivyo vya ulinzi wa mazingira, mauatumaini yapo kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi mtendaji wa UNEP Joyce Msuya.” Wakati mwaka 2018 ulikuwa na changamoto nyingi tumeshuhudia ongezeko la hatua na uwajibikaji wa kimataifa za kuingia katika njia mpya za kufanya mambo ambayo yatakabiliana na changamoto tulizonazo. Jukumu letu katika kutanabaisha njia bora, kuchagiza hatua na kuwaleta pamoja wadau ambao ni serikali, asasi za kiraia na sekta za biashara, kwa mara nyingine imethibitika kuwa muhimu sana.”

Ripoti hiyo iliyotolewa mtandaoni katika kuelekea Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEA 2019 inaonyesha kwamba kasi ya kuchukua hatua katika masualka mbalimbali uyanayohusiana na mazingira inaongezeka.

UNEP inasema siku ya Mazingira duniani 2018 ilihamasisha hatua dhidi ya uchafuzi utokanao na plastiki na kuwafikia mamilioni ya watu katika nchi Zaidi ya 190, huku India ikiahidi kukomesha kabisa matumizi ya mara moja ya plastiki ifikapo 2022.

UNEP imeshirikiana na shirika la afya duniani WHO kuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu uchafuzi wa hali ya hewa ambao hukatili Maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka , huku mashirika hayo yakizisaidia nchi kuboresha ubora wa hewa wavutayo kwa kupitia usafiri unaotumia nishati ya umeme, matumizi bora ya mafuta na mbinu zingine.

Mashirika, nchi na UNEP walikuja pamoja ili kulinusuru bonde la Congo ambalo ni maskani ya aina 14 ya viumbe vilivyoko thatarini kutoweka duniani na muhifadhi wa hewa ukaa ambayo ni sawa na gesi ya miaka mitatu inayozalishwa viwandani kimataifa .

Pia ripoti hiyo inaonyesha juhudi za UNEP na matunda yake katika maeneo mengine kama kuzisaidia jamii Darfur kupunguza migogoro ya rasilimali wakati huu wa mabadiliko ya tabia nchi na kuzielimisha mamlaka ili ziweze kutilia mkazo sharia za mazingira.