Macedonia

Kukata tamaa sio hulka yangu: Nimetz

Mwezi Juni mwaka jana mkataba wa kihistoria ulimaliza mgogoro wenye utata wa miaka 27 kati ya nchi mbili, ambazo ni jamhuri ya Yugoslavia ya zamani na Ugiriki.

Sauti -
4'16"

Kukata tamaa sio hulka yangu: Nimetz

Mwezi Juni mwaka jana mkataba wa kihistoria ulimaliza mgogoro wenye utata wa miaka 27 kati ya nchi mbili, ambazo ni jamhuri ya Yugoslavia ya zamani na Ugiriki. Mwanaume mmoja Matthew Nimetz kwa uvumilivu na hekma aliongoza majadiliano kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miongo miwili na akizungumza na UN News amesema Imani yake ya matokeo chanya katika mchakato huo haikuwahi kutoweka.

Umoja wa Mataifa wazipongeza Ugiriki na Macedonia kumaliza mgogoro wa tangu mwaka 1991.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepokea taarifa rasmi ya utekelezaji wa makubaliano ya Prespa ambayo yanafanya kufikiwa muafaka wa kuanza kutumika kwa jina la Jamhuri ya Marcedonia Kaskazini, taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imeeleza.

Mgogoro wa jina kati ya Ugiriki na Macedonia iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia unaelekea kupata suluhu: UN

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa jina katika ya Ugiriki na Macedonia iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia (FYROM), Matthew Nimetz, amepokea uamuzi wa bunge la Jamhuri hiyo ya zamani ya Yugoslavia wa kupitisha makubaliano kuhusu jina jipya la nchi hiyo kufuatia mgogoro ambao umedumu kwa miaka 28.