Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ustawi wa jamii kwa watoto ni haki ya binadamu:UNICEF/ILO

Watoto wakiwa Nepal wanauza maua Durbar Square, Kathmandu
UN News/Eric Ganz
Watoto wakiwa Nepal wanauza maua Durbar Square, Kathmandu

Ustawi wa jamii kwa watoto ni haki ya binadamu:UNICEF/ILO

Haki za binadamu

Ulinzi wa ustawi wa jamii kwa watoto ni haki ya binadamu ya kimataifa na kila nchi inapaswa kuhakikisha hilo, imesema ripoti ya pamoja iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la kazi duniani ILO.

Ripoti hiyo ya pamoja “kuelekea ulinzi wa kimataifa wa kijamii kwa watoto”  ambayo lengo lake ni kuhakikisha watoto wanahepa umasikini inasema licha ya kwamba ulinzi wa ustawi wa jamii ni haki ya wote theluthi mbili ya watoto wote duniani sawa na watoto bilioni 1.3 hawapati ulinzi huo na idadi inatofautia kikanda ambapo bara Ulaya na Asia watoto wanaopata baadhi ya ulinzi wa ustawi wa jamii ni hadi asilimia 88 wakati Afrika ni asilimia 16 tu. 

Akisisitiza umuhimu wa ulinzi huo wa ustawi wa jamii kwa watoto Elizabeth Ortis mkurugenzi wa kitengo cha ulinzi wa huduma za ustawi wa jamii katika shilika la Ilo amesema

(SAUTI YA ELIZABETH ORTIS)

“Hivyo ni dhahiri kwamba kuna mapengo mengi na ni muhimu sana kutambua kwamba ni haki ya binadamu ustawi wa jamii kwa watoto wote , na hii inamaanisha kwamba kuna uwekezaji mdogo sana kwa watoto.”

Kwa mujibu wa ripoti watoto wote kuanzia umri 0 hadi miaka 14 ambao ni sawa na asilimia 25 ya watu wote duniani , ni asilimia 1.1 pekee ya pato la dunia ndio lililotengwa kwa ajili ya huduma za ustawi wa jamii kwa ajili ya watoto. Hivyo Elizabeth anasema

(SAUTI YA ELIZABETH ORTIS CUT 2)

“Kuna pengo kubwa la uwekezaji ambalo linatakiwa kuzibwa, na idadi inakuwa mbaya zaidi tunapoenda kikanda , kwa mfano Afrika watoto wanawakilisha asilimia 40 ya watu wote , lakini ni asilimia 0.6 tu ndio uwekezaji uliotengwa kwa ajili ya ulinzi wa ustawi wa jamii kwa watoto.”

Ripoti hiyo imezitaka nchi kuangalia upya hatua zake za kukabiliana na changamoto za kiuchumi zisikandamize haki ya watoto kulindwa kijamii na kupata ustawi kwa masuala kama elimu, afya, lishe na huduma zingine za msingi.

Naye David Stewart ambe ni mkuu wa kitengo cha umasiki, watoto na ulinzi wa ustawi wa jamii wa UNICEF amesema umasikini unaowaghubika watoto hivi sasa duniani nio suala muhimu la kulishughulikia

(SAUTI YA DAVID STEWART)

“Kuna watoto milioni 385 dunaini wanaoishi katika umasikini wa chini ya dola moja na senti 90 kwa siku , na mara nyingi idadi hiyo wataendelea kuishi katika mazingira ya fecha kidogo ambayo hayawaruhusu kufikia kilele cha uwezo wao, watoto wanauwezekano mara mbili zaidi ya kuishi katika umasikini kama watu wazima.”

Ameongeza kuwa hili linaathari kubwa sio kwa watoto tu bali pia kwa jamii. Hivyo ripoti imependekeza kupanua wigo wa masuala ya ustawi wa jamii kwa watoto ikiwemo mfumo wa kimataofa wa ustawi wa jamii ambao utawalinda watoto, kutengwa fungu maalumu la fecha kushughulikia huduma muhimu kama elimu, afya, lishe na uhakika wa chakula.