Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake bado wanalipwa ujira mdogo kuliko wanaume duniani:ILO

Ripoti ya ILO ya pengo la mishahara 2018/19 imebaini kwamba wanawake bado wanalipwa asilimia 20 pungufu ya wanaume
© ILO/Marcel Crozet
Ripoti ya ILO ya pengo la mishahara 2018/19 imebaini kwamba wanawake bado wanalipwa asilimia 20 pungufu ya wanaume

Wanawake bado wanalipwa ujira mdogo kuliko wanaume duniani:ILO

Haki za binadamu

Ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO  kuhusu kiwango cha mishara inaonyesha kuwa ongezeko la mishahara kote duniani kwa mwaka 2017 lilikuwa  chini sana tangu mwaka 2008 na wanawake bado wanalipwa ujira mdogo kuliko wanaume. 

Ripoti hiyo “kiwango cha mishahara 2018-2019”, iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis na shirika la kazi duniani ILO, inasema duniani kote kiwango cha mishahara kilishuka hadi asilimia1.8 mwaka 2017 kutoka asilimia 2.4 mwaka wa 2016, kutokana na  takwim zilizokusanya kutoka mataifa 136 .

Ripoti pia ikifafanua kuhusu pengo hilo la mishahara kimataifa imnasema imebaini kwamba wanawake wanaendelea kulipwa takribani asilimia 20 pungufu ya wanaumme. Na lkwa nchi zilizoendelea pengo hilo liko bayana kwenye kazi zenye malipo makubwa wakati katika nchi za kipato cha nini pengo kubwa la mishahara liko katika kazi za ujira mdogo.

Kwa mujibu wa Ushahidi uliokusanywa na ripoti hiyo sababu zilizozoeleka kama tofauti za viwango vya elimu kati ya wanawake na wanaume ambao wanafanya kazi na kupipwa zinanafasi ndogo sana katika pengo hilo la mishahara baina ya wanawake na wanaumme. Rosalia Vazquez-Alvarez , ni mwanauchumi wa ILO na mtaalam wa mishahara.

 (SAUTI YA RASALIA VAZQUEZ )

“Kimsingi  uzalishaji waajira  umeshuka  kidogo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita huku kiwango cha mishahara kimebaki palepele hivyo pengo kati ya ongezeko la ajira na mshahara bado viko kiwango kilekile.”

Mkurugenzi Mkuu wa ILO,Guy Ryder amesemaa kinachoshangaza zaidi ni kwamba licha ya kupanda kwa pato la taifa la GDP na idadi ya wasio na kazi kushuka pengo bado liko bayana baina ya wanaume na wanawake katika mishahara.