Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumesalia bila chochote isipokuwa ndoto zetu:Wakimbizi wa Palestina

Atef A-nimnim na familia yake katika kambi ya wakimbizi wa kipalestina walioko Gaza
UN News/Reem Abaza
Atef A-nimnim na familia yake katika kambi ya wakimbizi wa kipalestina walioko Gaza

Tumesalia bila chochote isipokuwa ndoto zetu:Wakimbizi wa Palestina

Wahamiaji na Wakimbizi

Maelfu ya wakimbizi wa Kipalestina wanaoshi Ukanda wa Gaza wanasema hawana chochote, hata matumaini yameanza kupotea sipokuwa ndoto zao. Hii ni kutokana na madhila na machafuko ya miaka nenda rudi katika eneo hilo linalokaliwa na Israel. Wengi wanaishi wanaishi makambini ikiwemo kambi ya Al-Shati

NATTS…..UMM IHAB

Ni sauti ya Umm Ihan mwenye umri wa miaka 45 akijitambulisha na kusema anaishi kwenye nyumba ndogo ya mita 60 tu na mbovu  kambini hapo na jwatu wengine 13 wa familia yake akiwemo mumewe.

(Sauti UMM IHAB)

“Angalia chumba hiki, angalia mlango mvua inaponyesha nyumba inafurika, Watoto wangu wote wanalala hapa, mtoto wangu wa kiume ana miaka 27 analala nje ya chumba, na mwingine wa kiume wa miaka 18 analala jikoni, hali nyumbani kwangu ni nimekuwa nikiteseka kwa zaidi ya miaka 20.”

Licha ya adha hiyo hofu kubwa ya Umm si malazi, bali ni wanae, mkubwa wa kiume anataka kuondoka Gaza na mvula mdogo ana ndoto za kwenda kusaka maisha bora kwa ajili yake na familia yake nje ya Gaza.

Na hivi sasa mumewe Al-Nunem ni mgonjwa, huku mwanaye wa kike anataka kuacha shule. Yote haya yanamchanganya na hofu kubwa ni ukata unaolikabili shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA ambalo ndio limekuwa tegemeo lao, sasa likishindwa kuwasaidia anasema itakuwa ni hukumu ya kifo kwao. Hali hii mmefanya mumewe Umm  aitwaye kuafiki wazo la mtoto wao mkubwa wa kiume Ehab la kutaka kuondoka Gaza lakini Umm analipinga vikali akipishana na mumewe

(SAUTI UMM NA MUMEWE)

Umm-Eh mola tafadhali waondolee madhila vijana wetu

Al-Nunem:Tafhadhali msaidie mwanangu aweze kusafiri nje ya Gaza

Umm:Sitaki asafiri kwa kuwa unaumwa, nini kitatokea chochote kikikupata? Sitaki aondoke

Al-Nunem:Nataka aende akajitengenezee maisha, ni bora aharibu maisha yake kwa ajili yangu? Ni ama apate kazi au asafiri.

Na suala hilo la ajira ndio mtihani mkubwa Gaza. Hata hivyo hali hiyo haijazima ndoto za Ehab

(SAUTI YA EHAB)

“Bado niña matumaini, sijawahi kupoteza matumaini maishani mwangu na mungua anajua Niko kama mlima, lakini wakati mwingine mtu anahisi kama mabawa yake yamevinjika…nataka kufanya kazi na kusaidia lakini hakuna fursa za ajira, mtu unaishije katika hali hii?”

Ehab hayuko peke yake kwani kwa mujibu wa UNRWA vijana 7 kati ya 10 Gaza hawana ajira , na kwa zaidi ya muongo mmoja Ukanda wa Gaza umekuwa chini ya shinikizo na vizuizi vilivyoweka na malaka ya Israel hali inayozidisha adha kwa mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina.