Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatma ya mamilioni ya Wapalestina inategemea ukarimu wenu nchi wanachama:UN

Wanafunzi wa Kipalestina wakiwa darasani wakinyoosha mikono kujibu maswali katika moja ya shule zinazoendeshwa na UNRWA Gaza
UN Photo/Shareef Sarhan
Wanafunzi wa Kipalestina wakiwa darasani wakinyoosha mikono kujibu maswali katika moja ya shule zinazoendeshwa na UNRWA Gaza

Hatma ya mamilioni ya Wapalestina inategemea ukarimu wenu nchi wanachama:UN

Msaada wa Kibinadamu

Mamilioni ya Wapalestina wanategemea shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kilapestina UNRWA, ili kula , kulala na kuishi na UNRWA haiwezi kukidhi mahitaji hayo endapo nyinyi nchi wanachama na wadau wengine hamtoonyesha ukarimu kwa kunyoosha mkono zaidi kuisaidia

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza kwenye mkutano wa Baraza Kuu wa kuchangisha fedha kwa ajili ya UNRWA  amesema “inasikitisha kwamba hadi sasa suluhu ya kisiasa haijafikiwa ambayo itakidhi matakwa na matarajio ya wote Wapalestina na Waisrael. Narejea kusisitiza umuhimu wa kuelendelea na juhudi za amani za kuhakikisha kunapatikana suluhu ya mataifa mawili Israel na Paletina ambayo yataishi kwa pamoja kwa amani na usalama.”

Msaada wa UNRWA kwa Wapalestina

Ameongeza kuwa kwa takribani miongo saba sasa UNRWA imekuwa ikiwasaidia wakimbizi wa Kipalestina na inaendelea kufanya hivyo hadi suluhu ya kudumu itakapopatikana. Lakini sasa inakabiliwa na changamoto kubwa ya fecha kuweza kukidhi mahitaji ya msingi ya wakimbizi hawa hivyo natoa wito kwamba kazi ya UNRWA ionekane sio tu jukumu letu la pamoja bali mafanikio yetu ya pamoja.

Binti Hanan Abu Asbeh mwenue umri wa miaka 14 kutoka Ukingo wa Magharibi na kijana Hatem Hamdouna kmwenye umri wa miaka 15 kutoka Gaza wakihutubia Baraza Kuu mjini New York katika mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya UNRWA na kuelezea maisha yao kamf
UN Photo/Manuel Elías
Binti Hanan Abu Asbeh mwenue umri wa miaka 14 kutoka Ukingo wa Magharibi na kijana Hatem Hamdouna kmwenye umri wa miaka 15 kutoka Gaza wakihutubia Baraza Kuu mjini New York katika mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya UNRWA na kuelezea maisha yao kamf

Mwisho wa mwezi huu UNRWA inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha ambao utazuia kutoa msaada kwa wakimbizi milioni 5.4 na kutishia elimu kwa watoto 500,000, huduma za afya kwa watu milioni 8 kwa mwaka lakini pia msaada wa dharura kwa Wapalestina milioni 1.5.”

Katibu Mkuu pia amegusia hatua zilizochukuliwa na UNRWA katika kupunguza matumizi na katika miaka mitano iliyopita shirika hilo limeweza kutoa dola milioni 500 kupitia mabadiliko iliyofanya lakini pia kupanua wigo wa wafadhili .

Hali halisi kwa Wapalestina

Miongoni mwa walioshiriki katika mkutano huu ni vijana wawili wa umri wa miaka 14 wanafunzi Hanan na Hatem wakiwakilisha bunge la wanafunzi wa Gaza na Ukingo wa Maghharibi ambao kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa msaada wa UUNRWA kwa maisha yao, ya familia zao na mustakbali wa mamilioni ya watoto katika eneo hilo ambao elimu yao, lishe yao na mustakabali wao unategemea kuendelea kutoa msaada kwa shirika la UNRWA. 

Wamewasihi wahisani kuendelea kunyoosha mkono na kuichangia UNRWA wakisema “Msaada wenu sio tu kwa ajili yetu leo bali pia kwa taifa la kesho la Palestina na bila UNRWA maisha yetu, uhai wetu na mustakabali wetu uko njia panda.”

Mradi wa dharura kwa elimu ulio chini ya shirika la UN la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA husaidia pia kampeni ya mwaka ya watoto kurejea shule muhula mpya wa masomo unapoanza mwezi Septemba.
UNRWA/Rushdi El-Saraaj
Mradi wa dharura kwa elimu ulio chini ya shirika la UN la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA husaidia pia kampeni ya mwaka ya watoto kurejea shule muhula mpya wa masomo unapoanza mwezi Septemba.

 Naye Kamishina mkuu wa UNRWA Pierre Krahenbuhl amesisitiza umuhimu w anchi wanachama kuendelea kuchangia URWA kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya dharura ya Wapalestina amesema “kwa mamlioni ya wakimbizi wa Palestina hawana pa kugeukia wala pa kushika hatma yao iko mikononi mwa UNRWA na shirika hili halitoweza kunusuru maisha ya watu hao katika huduma za msingi kama chakula, malazi, huduma za afya na elimu endapo haitokuwa na fedha zinazohitajika. Nawasihi kuongeza msaada wenu sio tu kwa ajili ya sasa bali kwa mustakabali wa taifa la Palestina ka vizazi vyake.”

UNRWA ilianzishwa mwaka 1949 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa kutoa msaada wa kibinadamu na ulinzi kwa wakimbizi wa Kipalestina walioorodheshwa Jordan, Syria, Lebanon, Gaza na Ukingo wa Magharibi ikiwemo Jerusalem Mashariki.

Shirika hilo ambalo linafadhiliwa kwa mchango wa hiyari w anchi wanachama , liliweza kuziba pengo la dola milioni 446 mwaka 2018 kutokana na ukarimu mkubwa wa msaada kutoka kwa nchi wanachama na dola milioni 92 ambazo zilitokana na kubana matumizi kwa UNRWA. Pengo la ufadhili limechangiwa kwa kiasi kikubwa na Marekani kupunguza ufadhili wake kwa shirika hilo.