Timisoara, ni makazi ya muda ya wakimbizi walio njiani kuelekea nchi ya tatu.

31 Januari 2019

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM wanaendelea na harakati za kuwahamisha wakimbizi kutoka Libya ambao sasa wamekuwa wageni wa muda wa serikali ya Romania kwenye  kituo cha ETC kilichoko mjini Timisoara Romania .

ETC ni makazi ya muda ya wakimbizi walio safarini kusaka usalama katika nchi ya tatu.  Wakimbizi hao wanapelekwa nchini Norway kwa ajili ya kupatiwa makazi ya kudumu.

Mjane Hawa na watoto wake sita walikimbia vita Darful Sudan wakaingia Libya na kwa bahati mbaya wakakuta Libya imeghubikwa na machafuko.

“Baba yao alifariki. Kitu pekee ninachokitaka kwa ajili yao ni elimu bora na makuzi mema”

Jumla ya wakimbizi 51 kutoka Sudan, Eritrea na Syria waliuokuwa Libya walifika Romania kwa ndege ya abiria iliondoka mjini Tripoli mapema Disemba 5 ikipita Istanbul na Bucharest na kuwasili mjini Timisoara tarehe 6.

Mohamed, mtoto wa kiume wa Hawa alisomea udaktari nchini Libya lakini vita na kukosekana kwa usalama vikazima ndoto zake.

“Hakuna la kufanya tukibaki nchini kwetu, hakuna lolote, sina kazi, si masomo. Hakuna maisha”

UNHCR inafanya juhudi kubwa kuwaondoa nchini Libya wakimbizi walioko hatarini kisha inachambua waliko hatarini zaidi kama wanawake, Watoto yatima na walioteswa na kujaribu kuwatafutia nchi za kuwapokea kama Norway na Uingereza na wakati wanasubiri kupokelewa wanafundishwa lugha na utamaduni.

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter