Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Filamu "Capernaum" kuhusu wakimbizi na wahamiaji yashindania tuzo za Oscars 2019

Mtoto Zain, mkimbizi kutoka Syria wakati akiwa Lebanon akijiandaa kwa safari yake ya kuhamia Norway
© UNHCR/Sam Tarling
Mtoto Zain, mkimbizi kutoka Syria wakati akiwa Lebanon akijiandaa kwa safari yake ya kuhamia Norway

Filamu "Capernaum" kuhusu wakimbizi na wahamiaji yashindania tuzo za Oscars 2019

Wahamiaji na Wakimbizi

Nadine Labaki, mwongoza filamu kutoka Lebanon ambaye filamu yake ya Capernaum imechaguliwa kushindania tuzo ya Oscar kwa mwaka huu wa 2019 katika kipengele cha filamu za lugha ya kigeni, amezungmzia kile kilichomfanya kuandaa filamu hiyo inayohusu madhila yanayokumba mamilioni ya watu duniani katika zama za sasa ikiwemo  ukimbizi na uhamiaji.

Sauti hiyo ya Zain Al Rafeea mtoto mkimbizi kutoka Syria ambaye ni muigizaji mkuu katika filamu hiyo ya Capernaum, au ‘Vurumai’ ambamo kisa kikubwa kinachomhusu ni kuwashtaki mahakamani wazazi wake kwa kosa tu la kumleta duniani, akijikuta ukimbiziniLebanon na kuishia kufanya kazi za suluba.

Akihojiwa na Idhaa ya kiarabu ya Umoja wa Mataifa, Nadine Labaki, mwongozaji wa filamu hiyo anasema madhila yanayokumba wakimbizi kama Zain, ndio yalimsukuma kufanya filamu hiyo na asingalifanya hivyo basi ingalikuwa sawa na kutenda uhalifu kwa sababu watoto, "wanafanya kazi mitaani kulisha familia zao, wanafanya kazi katika mazingira magumu, na huwezi kujizuia kuzungumzia machungu hayo. Na niliamua kuzungumzia hilo kupitia mtazamo wa mtoto.”

Mtoto Zain, mkimbizi kutoka Syria wakati akiwa Lebanon akijiandaa kwa safari yake ya kuhamia Norway
© UNHCR/Sam Tarling
Mtoto Zain, mkimbizi kutoka Syria wakati akiwa Lebanon akijiandaa kwa safari yake ya kuhamia Norway

Nadine akafafanua sababu ya kutumia watoto akiwemo Zain, "mtoto anaona mambo kwa mtazamo wa wazi zaidi kuliko mtu mwingine kwasababu anakuwa hajapatiwa mtazamo wa jamii, unafiki au siasa.”

Mtoto Zain hivi sasa amepata hifadhi kwenye nchi ya tatu Norway na filamu yao ya Capernaum mwaka jana ilishinda tuzo kwenye tamasha la filamu la Cannes, Ufaransa.