Mtoto mkimbizi wa Syria huko Lebanon kupata cheti cha kuzaliwa kwa urahisi
Mabadiliko muhimu yaliyofanyika katika utaratibu wa sheria za Lebanon kuhusu usajili wa watoto umewezesha zaidi ya watoto 50,000 wakimbizi kutoka Syria waliozaliwa Lebanon tangu mgogoro uanze nchini mwao kuweza kusajiliwa.
Kusini mwa Lebanon katika moja ya kambi za wakimbizi wa Syria.
Awali watoto wa wakimbizi wa Syria waliozaliwa hapa Lebanon na kukosa kusajiliwa ndani ya mwaka mmoja baada ya kuzaliwa, walipata taabu kupata cheti cha kuzaliwa.
Wazazi walipaswa kulipa hadi dola 1,500 ili kupata cheti, gharama ambayo ni ya juu na hawakuipatia umuhimu kutokana na mahitaji mengine ya lazima.
Watoto walikosa huduma muhimu kama afya na elimu.
Mohammad al-Masry ni mkimbizi kutoka Syria.
“Siwezi kufanya lolote kwa ajili ya mwanangu kisheria bila ya kitabu cha familia. Inanilazimu kufanya hivyo nchini Syria , lakini ni vigumu kwenda huko hivi sasa.”
Hata hivyo hivi karibuni serikali ya Lebanon ilipitisha uamuzi ya kwamba watoto wote wa Syria waliozaliwa kati ya Januari Mosi 2011 na mwezi Machi 2018 wasajiliwe bila gharama yoyote.
Mohammad Jarjowi, ni afisa wa sheria wa kamati ya kimataifa ya uokozi IRC.
“Sasa tunaweza kutayarisha vyeti vya kuzaliwa na kuvisajili katika masjala ya kigeni hata pale ambapo mtoto alikuwa amepitisha ukomo wa usajili wa ndani ya mwaka mmoja tangu azaliwe.”
Hatua hii imeokoa wakimbizi wengi kutoka Syria ambao watoto wao wamezaliwa ukimbizini Lebanon baada ya vita kuanza nchini mwao 2011.
Firaz ni mmoja wao na binti yake Yara Mimas ana umri wa miaka minne, kwake yeye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limemletea nuru.
“UNHCR ilinisaidia kumsajili binti yangu binti yangu Yara. Usajili wake ulishakuwa umepitiliza kwa miaka mitatu.