Hatari wapatazo wahamiaji watoto zawekwa dhahiri Marrakech

8 Disemba 2018

Kuelekea mkutano kuhusu mkataba wa kimataifa wa uhamiaji huko Marrakech Morocco wiki ijayo, Umoja wa Mataifa umeangazia hatari wanazokumbana nazo vijana wanaohamahama hususan wanapokuwa safarini.

Masuala hayo yameangaziwa wakati wa msururu wa vikao vinavyofanyika huko Marrakech.

Miongoni mwa vikao hivyo ni kile kilichofunguliwa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji wa kimataifa, Louise Arbour kikiangazia sera za uhamiaji ambapo amesema
“moja ya misingi ongozi ya mkataba huo wa kimataifa wa uhamiaji salama na unaofuata knuni ni kuendeleza wajibu wa kimataifa kuhusu haki za mtoto na umuhimu wa kuzingatia misingi hiyo wakti wote.”

Kwa mujibu wa kura ya maoni iliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, takribani nusu ya wakimbizi na wahamiaji 4,000 wenye umri wa kati ya miaka – 14 hadi 24 walioshiriki walisema walilazimika kukimbia nchi zao ilhali asilimka 44 walifanya hivyo bila ushawishi.

“Ilhali wanasiasa wanahaha kuhusu uhamiaji, watoto 4,000 wanasema wanataka usaidizi zaidi,” amesema Laurence Chandy, Mkurugenzi wa data, utafiti na sera UNICEF.

Bwana Chandy anasihi serikali zihakikishe uhamiaji ni salama kwa kuridhia mkataba wa kimataifa wa uhamiaji, GCM, na ahadi ambazo zinaelezwa ndani yake.

 “Uhamiaji haukwepeki, lakini hatari na ubaguzi ambao wanakumbana nazo wahamiaji na wakimbizi watoto havipaswi kuwa hivyo,” amesema Bwana Chandy.

Katika jitihadq sa kuangazia zaidi madhila ynayokumba wahamiaji, UNICEF iliungana na serikali ya Morocco bayo ni mwenyeji wa mkutano huo na kufungua maonyesho ya sanaa yaitwayo ‘Safari kama mhamiaji kijana: Kuleta simulizi kupitia sanaa.’

Kader, mhamiaji kijana kutoka Côte d’Ivoire, alielezea uzowfu wake wa kusafiri peke yake, kupitia njia hatari zaidi hadi Italia ambako sasa amehamia.

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa UN kwa vijana Jayathma Wickramanayake alishiriki ufunguzi na kuelezea jinsi picha za sanaa zinazoonyeshwa zinavyoelezea dhahiri madhila kama aliyoshuhudia huko Cox’s Bazar kwa wakimbizi kutoka Myanmar.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter