Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unaweza kubeba mkoba uliotengenezwa kwa ngozi ya samaki?

Mkoba uliotengenezwa kutokana na ngozi ya Samaki
Video Capture/Unifeed
Mkoba uliotengenezwa kutokana na ngozi ya Samaki

Unaweza kubeba mkoba uliotengenezwa kwa ngozi ya samaki?

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Nchini Kenya harakati za shirika la chakula na kilimo duniani, FAO la kuchaguzi matumizi bora ya rasilimali za bahari zimezaa matunda baada ya wajasiriamali kuitikia wito na kutumia ngozi ya samaki aina ya sangara kutengeneza bidhaa za kibiashara. 

Ni eneo la Kitale huko Eldoret nchini Kenya katika kiwanda cha minofu ya samaki cha Victorian Foods, wafanyakazi wakiandaa samaki aina ya sangara kwa ajili siyo tu ya minofu yake bali pia ngozi yake.

Mfanyakazi akiwa na glovu na brashi anasafisha na kupaa samaki huyu… kisha ni hatua ya kutoa mnofu na ngozi inayosalia inasafishwa na kupitia mchakato mzima hadi inakaushwa.

Ngozi ya sangara kwa muda mrefu imekuwa tatizo kubwa kwani ilionekana ni taka, lakini sasa ni mali na hii inatokana na mpango wa FAO wa kuongeza thamani kwa rasilimali za bahari kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii au Blue Growth ulioanza mwaka 2013.

James Ambani, ni afisa mtendaji mkuu wa Victorian Foods

 “Ngozi ya samaki inaonekana ni ya kianasa, kama ya nyoka na unajua nyoka ni viumbe vilivyoko hatarini kutoweka kwa hiyo ngozi mbadala ni ya samaki. Na hii huhitaij kibali cha kuuza nje. Naamini kadri inapata umaarufu, mahitaji ya soko yataongezeka.”

Tayari ngozi hii ya sangara imetumika kutengeneza makobazi, mabegi, pochi na yaelezwa kuwa ngozi hii inadumu sana na tayari wabunifu wa nguo nchini Kenya, kama Jamil Walji, wanaitumia.

“Nilipata msukumo wa kuchanganya ngozi hii pamoja na kanga na vitambaa kutoka Ulaya. Nataka kuleta mchanganyiko ambao haujawahi kutokea.”

Ngozi ya Samaki inatumika katika tasnia ya mitindo.
Video Capture/Unifeed
Ngozi ya Samaki inatumika katika tasnia ya mitindo.

Na sasa ni maonyesho ya mitindo ya nguo na jukwaani wanaonekana walimbwende wakiwa wamevalia mavazi yenye mchanganyiko wa kanga na ngozi ya sangara na  biashara katika sekta hii ya ngozi ya sangara ndio yanashika kasi.

TAGS: Sangara, Blueeconomy, FAO, Kenya, Victorian Foods, Sangara