Mradi wa pamoja wa shirika la chakula na kilimo FAO na serikali ya Kenya wa kutoa onyo mapema kuhusu majanga umesaidia wafugaji kukabiliana na ukame na kuepusha njaa na vifo.
Pande mbili hizo zilitiliana saini makubaliano hayo mwezi disemba mwaka 2016 baada ya kudhihirika kuwa Kenya itakabiliwa na ukame mkali utakaosababisha njaa kwa watu milioni 1.3 na vifo vya mifugo yao.
Kupitia mradi huo FAO ilitoa dola 400,000 kwa lengo la kuwezesha wafugaji kupata malisho ya mifugo yao hata wakati wa ukame na hatimaye kuepusha vifo vya mifugo na wakati huo huo watoto kupata lishe bora ya maziwa.
FAO inasema wafugaji zaidi ya 12,800 walipata chakula cha mifugo yao na Mlongo Mwanyasi ni mmoja wa wanufaika.
(Sauti ya Mlongo Mwanyasi)
Mnufaika mwingine ni Harrison Kazungu Karisa
(Sauti ya Harisson Kazungu Karisa)
FAO inasema kwa kila dola moja iliyotumika kuokoa mifugo, kaya ilijipatia dola 3.5, hali ambayo imesema ni dhahiri kuwa mfumo wa kutoa onyo mapema kuhusu majanga ni uwekezaji ulio na tija.