Kuna haja ya kuamsha ari ya utekelezaji wa tamko la haki za binadamu-UN

7 Disemba 2018

Wataalamu huru wa haki za binadamu  wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza haja ya kuamsha tena ari ya utekelezaji wa tamko la haki za binadamu lililozinduliwa yapata miaka 70 iliyopita.

Katika taarifa ya kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya tamko hilo iliyotolewa na wataalamu hao wanaoteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu wamesema ingawa kuna mafanikio mengi duniani tangu kupitishwa kwa tamko hilo ikiwemo kushuhudia maendeleo ya kukua kwa viwango vya haki za binadamu katika nchi mbalimbali duniani lakini bado kuna changamoto nyingi katika utekelezaji wa tamko hilo kwani wamesema “Leo hii tunashuhudia vita, machafuko na ukiukwaji wa utu wa binadamu kila siku katika sehemu mbalimbali duniani, baadjhi ya nchi na viongozi wa kisiasa wakijihusisha na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.”

Taarifa yao imeongeza kuwa mifano ya karibuni ni mauaji ya kimbari, uhalifu wavita unaoendelea katika migogoro mbalimbali,uhalifu dhidi ya ubinadamu na ukwepaji wa sheria ukishamiri katika nchi nyingi zilizoghubikwa na vita vinavyoendelea au machafuko ya kisiasa ukichangiwa na malengo ya kitaifa, siasa na changamoto za kisiasa kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Msataifa.

Wataalamuhao wamesema kuna mambo mengi yanayodhihirisha mmomonyoko kwa utekelezaji wa tamko la haki za binadamu mbali ya vita kama vile changamoto kubwa hivi sasa ya uhamiaji iliyosababishwa navita, masuala ya kiuchumi, umasikini, utawala wa kiimla, chuki dhidi ya wageni, sera za utaifa na mengineyo hali inayosababisha kutia dosari mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushirikiano wa kibinadamu wa kimataifa kwa miaka takriban 70 iliyopita.

Wamesema nchi nyingi haziwatendei watu wote sawa kwa missing ya utu na usawa ulioainisha kwenye ibara za tamko hilo, hivyo wamekumbusha kwamba tamko hilo lilipitishwa baada ya migogoro kwa lengo la kumaliza na kudumisha amanihivyo ni muhimu kukumbuka mnepo wa ujumbe huona kuwa na haja ya kila mtu kutimiza ahai upya ya tamko hilo kwa miaka mingine 70.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter