Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu ya mataifa 2 bado ndio jawabu kwa Wapalestina:Guterres

Vifusi vya nyumba za waPalestina zilizobomolewa eneo la Beit Hanina, Jerusalem Mashariki.
UNRWA/Marwan Baghdadi
Vifusi vya nyumba za waPalestina zilizobomolewa eneo la Beit Hanina, Jerusalem Mashariki.

Suluhu ya mataifa 2 bado ndio jawabu kwa Wapalestina:Guterres

Haki za binadamu

Suluhu ya kuwa na mataifa mawili ambapo Israel na Palestina wataishi kama mataifa huru inasalia kuwa ndio njia pekee ya amani ya kudumu na kumaliza mzozo wa miaka na mikaka.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wau moja wa Mataifa Antonio Guterres Jumatano wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina.

Mwaka 1947 kwa pendekezo la Palestina Baraza Kuu lilipitisha Azimio namba 181, lakini hadi sasa taifa huru na lenye kujitawala halijaundwa.

Mr.Guterres ametoa wito kwa viongozi wa Palestina na Israel “kurejesha Imani ya ahadi ya azimio namba 181 , la mataifa mawili yatayokuwepo pamoja kwa amani na usalama na kutekeleza matakwa halali ya watu wao , huku wakiwa na mipaka inayotokana na mistari iliyowekwa mwaka 1967 na mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa maitfa yote mawili ambapo Jerusarem Mashariki  kuwa mji mkuu wa taifa la Palestina hi indio njia pekee ya kufikia haki zisizoweza kuondolewa za watu wa Palestina .”

Naye rais wa Baraza Kuu , María Fernanda Espinosa ameelezea jukumu la Umoja wa Mataifa katika mchakato wa amani. Ameikumbusha kamati na wote walioshiriki kuhusu kaulimbiu ya kikao cha 73 cha Baraza Kuu”Kuufanya Umoja wa Mataifa kuwa  wa maana kwa wote “ akisistiza kuwa “Mshikamano wetu na watu wa Palestina usiwe tu wa kutokana na huruma, kama ilivyo tahamani yao , Wapalestina wanastahili zaidi ya hilo na kuhakikisha hakuna anayesalia nyuma ni lazima tufanye kila lililondani ya uwezo wetu kukomesha jinamizi hili la sasa kwani haitoshi kupiga debe tu kwa ajili ya watu wa Palestina endapo hatuko tayari kutekeleza ari ya kisiasa inayohitajika kufanya msimamo huo uwe na maana.”

Akitoa wito kwa viongozi wa dunia rais huyo wa Baraza Kuu ametangaza haja yay a hatua za haraka kukabiliana na mgogoro wa muda mrefu wa kibinadamu uliotokana na miongo ya vita na kutoaminiana.

“Taifa la watu wa Palestina linasalia kuwa kovu katika wajibu wetu wa pamoja na wote tuna jukumu la kushinikiza haja ya haraka ya kupatikana kwa suluhu.”