Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watekelezaji wa mashambulizi ya kigaidi Nigeria wawajibishwe:Guterres:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

Watekelezaji wa mashambulizi ya kigaidi Nigeria wawajibishwe:Guterres:

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mashambulizi ya kigaidi  ya mara kwa mara yanayofanywa na makundi mengine yenye itikadi kali Kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifo na majeruhi miongoni mwa raia, vikosi vya usalama na kuvuruga utaratibu wa maisha ya kawaida.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake,  Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Nigeria na familia za waliopoteza maisha katika mashambulio hayo .

Duru za habari zinasema shambulio la kigaidi lilifanyika Ijumaa baada ya kundi linalojiita jimbo la kiislam la Afrika Magharibi, ISWA,  kushambulia kituo cha jeshi cha Metele Kaskazini mwa Nigeria na kukatili maisha ya wanajeshi 40.

Mapema leo Jumatatu wapigamaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram ambao ni sehemu ya kundi hilo la Kiislam wametangaza kutekeleza mashambulizi hayo. Akisisitiza kuhusu uwajibikaji , Katibu Mkuu amesema wote waliokiuka sharia kimataifa za kibinadamu , haki za binadamu na sharia za wakimbizi ni lazima wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.

Pia amesema Umoja wa Mataifa unashikamana na serikali ya Nigeria katika vita dhidi ya ugaidi na itikadi kali.