Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres aridhia kujiuzulu kwa Solheim, sasa Bi. Msuya kukaimu

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP Erik Solheim.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Guterres aridhia kujiuzulu kwa Solheim, sasa Bi. Msuya kukaimu

Masuala ya UM

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, Erik Solheim amejiuzulu wadhifa huo, hatua ambayo imeridhiwa na Katibu Mkuu Antonio Guterres.

 Habari zinasema kwamba Solheim raia wa Norway ambaye ameshika wadhifa huo kuanzia mwaka 2016, amejiuzulu baada ya ripoti ya ukaguzi ya Umoja wa Mataifa kubaini kuwa alitumia dola laki Tano za kimarekani kwa ajili ya safari, fedha ambazo hata hivyo wakati wa mrejesho hazikuwa na matumizi sahihi.

Kufuatia hatua hiyo ya kutangaza kujiuzulu, Katibu Mkuu Guterres kupitia msemaji wake, ameridhia uamuzi  huo wa Bwana Solheim akisema kuwa utaanza rasmi tarehe 22 mwezi huu wa Novemba na amemshukuru kwa mchango wake katika kusongesha harakati za uhifadhi wa mazingira duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric amesema kuwa Katibu Mkuu amemteua Naibu Mkurugenzi wa sasa wa UNEP, Joyce Msuya kutoka Tanzania kukaimu nafasi ya ukurugenzi mtendaji wa  UNEP wakati mchakato wa kumpata mtendaji mpya ukiandaliwa.