Vita visipokoma njaa itazidi kuwaangamiza Wayemen:WFP

Kutokana na kuzorota kwa hali ya kiusalama nchini Yemen, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linataka mapigano ya sasa katika mji wa bandari wa Hodeidah yakomeshwe mara moja kwani mbali ya kukatili Maisha ya watu yanayongeza idadi ya waathirika wa njaa linalowapa msaada wa chakula ,iliyopanda kutoka milioni 8 hadi milioni 14.
Katika barabara za mji wa Hodeidah uliosal;ia mahame nakujawa na vizuizi kadhaa barabarabani watu wengi wamefungasha virago kukimbia machafuko.
Kwa muda sasa mji wa Hodeidah umekuwa uwanja wa mapambano huku mahandaki yakionekana bayana barabarani . Hadi kufikia Juni mwaka huu wa 2018, takriban nusu milioni walikuwa wameuhama mji huo na wale walio baki maisha yao yako mashakani kutokana na mapigano yanayoendelea.
Bandari hiyo ndiyo uti wa mgongo wa Yemen kwani ndiyo njia pekee ya kuingizia chakula na mafuta ukizingatia kwamba asilimia 90 ya chakula cha Yemen kinatoka nje. Amer Daoudi ni Mkurugenzi mkuu wa operesheni wa WFP.
"Hodeidah inauwezo wa kumudu takriban asilimia 70 ya bidhaa zote zinzoingia Yemen kutoka nje , na endapo fursa hiyo haitokuwepo tutashuhudia zahma nchini Yemen na maisha ya watu yatakuwa hatarini . WFP inaongeza juhudi ili kuweza kutimiza mahitaji ya watu milioni 14 na Hodeidah ndiyo njia pekee muhimu kwetu kuweza kutimiza mahitaji ya watu hao.”
Na watoto wa Hodeidah ambako ndiko kwenye kiwango cha utapia mlo, wakati mwingine huwa dhaifu hata hushindwa kufungua vinywa kula chakula maalum wanachopewa kwa ajili ya kuimarisha lishe na siha yao.
Hivi sasa WFP inalenga kutoa chakula cha msaada kwa watu milioni 8 na bajeti yake ya dola milioni125 kwa mwezi itakuwa mtihani mgumu endapo fedha zaidi hazitopatikana kuhakikisha huduma hiyo ya lazima ya chakula inapatikana kwa maelfu ya watu wanaokabiliwa na njaa.