ISIL waliwazika pamoja maelfu ya watu : UN Ripoti

6 Novemba 2018

Makaburi zaidi ya 200 yakiwa na mabaki ya watu waliozikwa pamoja yamegunduliwa  katika maeneo kadhaa nchini Iraq

Katika ripoti ya Umoja wa Mataifa imetolewa leo mjini Geneva Uswisi na Baghdad nchini Iraq, makaburi hayo yamepatikana katikamaeneo ambayo zamani yalikuwa yanadhibitiwa na wapiganaji wa ISIL.

Ripoti inamulika utawalawa ISIL ambao uliendesha kampeni ya vitisho na ghasia pamoja na jinsi waathirika wanavyotaka kuwepo kwa ukweli na haki.

 Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq-UNAMI pamoja na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa zimeorodhesha  kuwepo makaburi makubwa 202 katika maeneo ya Ninewa,Kirkuk,Salah al-Din na Anbar katika maeneo ya kaskazini na magharibi mwa nchi. Hata hivyo huenda kukawa na makaburi mengine nchini humo.

 Mmoja wa manusura wa mauaji ya ISIL kutoka Kijiji cha Kocho wilaya ya Sanjir, anaeleza alishoshuhudia na kunusurika

(SAUTI YA MANUSURA)

“ Tulikuwa wanaume kati ya 30 na 40. Tulikuwa ndani ya magari matatu. Mmoja wao alikuwa akichukua picha zetu. kabla yakufika tuliona wapiganaji Da’esh watatu wakiwa wamesimama …mimi nilinusurika. Nilikaa kimya kwa muda wa dakika 15 hadi 30 bila  wala kupumua. Baadaye nikawaona  wakienda mahali pengine, niliinuka nikatoka nikakimbilia kwingine.”

Taarifa inasema huku ikiwa ni vigumu kujua idadi kamili ya watu walioko katika makaburi hayo,kaburi dogo  magharibi mwa Mosul, makaburi mengi yanakutwa na idadi kubwa ya maiti huku lililokuwa na watu wachache ni wananane.

Ripoti inasema kuwa ushahidi uliokusanywa ni muhimu katika mchakato wa kufanya uchunguzi ambao utasaidia kufungua mashtaka na baadaye kupata hukumu kwa kufuata mchakato wa viwango vya kimataifa.

 Ripoti inaendelea kuwa kati ya Juni mwaka wa 2014 na Disemba 2017 kundi la ISIL liliteka sehemu kubwa ya Iraq na kuendesha kilichoitwa kapeni kali iliyojaa ukiukwaji mkubwa wa haki za kimataifa za binadamu visa ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na uwezekano wa kuwa  mauaji ya kimbari.

 Ripoti pia imetoa mapendekezo kadhaa, miongoni mwa hiyo ni kuwa inataka kuchukuliwahatua mbalimbali kupata uashidi ikiwemo wa  wataaalm wa silaha na watalaam wa vilipuzi.    Pia inataka jamii ya kimataifa kutoa msaada wa vitendea kazi ili kusaidia kusafirisha mabaki ya wahanga, kuwatambua na pia kurejea mabaki hayo kwa familia zake.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud