Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto waliozaliwa kutokana na ukatili wa kingono Iraq lazima walindwe: UN

Madhila ya watoto nchini Iraq ni mengi kwa mfano huyu ni Sabreen aliyolazimishwa ndoa ya mapema wakati aliwasili kambi ya Domiz eneo la Kurdistan nchini Iraq.
UNFPA/David Brunetti
Madhila ya watoto nchini Iraq ni mengi kwa mfano huyu ni Sabreen aliyolazimishwa ndoa ya mapema wakati aliwasili kambi ya Domiz eneo la Kurdistan nchini Iraq.

Watoto waliozaliwa kutokana na ukatili wa kingono Iraq lazima walindwe: UN

Haki za binadamu

Naiomba serikali nchini Iraq kuhakikisha kwamba watoto waliozaliwa kutokana na wazai wao kubakwa wakati wa vita kuheshimwana kupewa ulinzi wa kisheria ili wasitengwe  na jamii na kunyanyapaliwa.

Ombi hilo limetolewa leo mjini Baghdad nchini Iraq na naibu wa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kisiasa na msaada katika  uchaguzi Alice Walpole, wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya kimataifa  ya kutokomeza ukatili wa kingono katika maeneo ya migogoro.

Bi Walpole amesema, "wanawake na watoto kwa kawaida ndio hubeba gharama kubwa  ya vita vya silaha. Na kwa wale walioishi chini ya utawala wa ISIL, mateso yalikuwa mara dufu. Hata hivyo mateso haya bado yanaendelea kwani mara nyingi watu hao wanatengwa na jamii na kuchukuliwa  kama washirika badala ya waathirika."

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza maadhimisho hayo kufanyika tangu majeshi ya serikali ya Iraq kuchukua tena udhibiti wa maeneo ambayo yalikuwa chini ya usimamizi wa kundi la wanamgambo wa ISIL.

Maadhimisho ya Iraq yalibeba kauli mbiu "taabu na haki kwa watoto waliozaliwa katika vita".

Bi Walpole ameoungeza mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq-UNAMI na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa nchini humo kwa kusaidia juhudi za serikali ya Iraq, kuimarisha  kujukumu la  kuwalinda watoto, kuwarejeshea heshima zao na pia kuwajumuisha tena katika jamii.

Naye mwakilishi wa shrika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF nchini Iraq, Peter Hawkins, amesema licha ya kuwepo mfumo wa kisheria unaowawezesha watoto kupata vitambulisho, lakini katika hali halisi ni mtihani kuvipata kwani mfumo kwanza unamtaka mamakuainisha hadharani aliyopitia, jambo ambalo  familia, utamaduni, kabila na kidini huyachukulia kama ni fedheha.

Ameongeza kuwa kumnyima mtoto kitambulisho inakwenda kinyume na misingi ya mkataba wa haki za watoto na kuna athari kubwa kwani mtoto huyo hawezi kupata huduma muhimu maishani kama vile elimu, huduma za afya na kadhalika bila ya kitambulisho.

Kwa upande wake, Naibu mjumbe wa UNFPA nchini Iraq, Nestor Owomuhangi, akizungumza kutoka eneo la Kurdistan, amesema watoto waliozaliwa kutokana na vitendo vya kubakwa au ndoa za lazima, kwa sasa wanakabiliwa na shida za kisheria na wanaweza kushawishika haraka kujiunga na makundi ya itikadi kali au kusafirishwa kiharamu, jambo ambalo lina athari mbaya kwa ulinzi na usalama wa taifa hilo.