Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

TEHAMA ina mchango mkubwa nchini Tanzania:Yonazi

Mkutano wa nchi wanachana wa muungano wa kimataifa wa mawasiliano, ITU
©ITU/D. Woldu
Mkutano wa nchi wanachana wa muungano wa kimataifa wa mawasiliano, ITU

TEHAMA ina mchango mkubwa nchini Tanzania:Yonazi

Ukuaji wa Kiuchumi

Mkutano wa nchi wanachana wa muungano wa kimataifa wa mawasiliano, ITU unaendelea mjini Dubai katika Falme za kiarabu kujadili mchango wa TEHAMA katika kuleta maendeleo duniani.

Mkutano huo wa wiki tatu ulioandaliwa na ITU utakakunja jamvi Novemba 16 na umewaleta pamoja wajumbe kutoka nchi wanachama, wataalamu wa TEHAMA, na wadau wengine wa maendeleo.

Mbali ya kuchagua viongozi unajadili sera na kusikiliza ripoti za nchi wanachama kuhusu hatua zilizopigwa katika TEHAMA na ufanikishaji wa malengo ya Mmaendeleo endelevu yaani SDG’s.

Jim Yonazi ni naibu Katibu Mkuu  katika wizara ya ujenzi , uchukuzi  na mawasiliano ya Tanzania amemueleza Flora Nducha wa Idhaa hii alichokiwasilisha mkutanoni.