Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya changamoto, Somalia imebadilika- Keating

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia , Michael Keating akikutana na baabdhi ya wasomali wahio unamishoni. Aema mgogoro pia umesasmbaratisha miundo mbinu ya nishati na kuvuruga mazingira.
Picha ya Umoja wa Mataifa
Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia , Michael Keating akikutana na baabdhi ya wasomali wahio unamishoni. Aema mgogoro pia umesasmbaratisha miundo mbinu ya nishati na kuvuruga mazingira.

Licha ya changamoto, Somalia imebadilika- Keating

Amani na Usalama

Kitendo cha vyombo vya habari kutoangazia mafanikio ni mojawapo ya sababu za watu hususan nje ya Somalia kutofahamu maendeleo yaliyopatikana nchini humo siku za karibuni na fursa zilizopo.

Ni kauli ya mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating ambaye anamaliza muda wake baada ya kushika wadhifa huo kuanzia  Januari Mosi mwaka 2016.

Akizungumza katika mahojiano maalum mjini Mogadishu, Somalia, Bwana Keating ametoa mfano wa uchaguzi wa rais uliofanyika na kuwezesha kipindi cha mpito kisicho na ghasia mwezi Februari mwaka huu, hatua iliyofuatiwa na uchaguzi wa wabunge.

(Sauti ya Michael Keating)

“Jambo la pili nadhani ni kuepuka njaa mwaka 2017. Nadhani mpito salama wa kubadilishana madaraka ya urais ulifanikisha hili. Jambo la kwanza ambalo rais alisema baada ya kuchaguliwa ni kwamba anataka kampeni ya kitaifa kushughulikia tatizo hilo na kujaribu kusaida wasomali walio kwenye shida, akihusisha jamii za ughaibuni, wafanyabiashara na jamii ya kimataifa.”

Rosemary DiCarlo, Mkuu wa idara ya siasa ya Umoja wa Mataifa (mwenye ushungi) akiwa na Michael Keating, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN nchini Somalia (kushoto) wakizungumza na Rais Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo kwenye ikulu ya Somalia Juni 7 2018.
UN / Omar Abdisalan
Rosemary DiCarlo, Mkuu wa idara ya siasa ya Umoja wa Mataifa (mwenye ushungi) akiwa na Michael Keating, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN nchini Somalia (kushoto) wakizungumza na Rais Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo kwenye ikulu ya Somalia Juni 7 2018.

Bwana Keating akataja hatua zilizochukuliwa na serikali ya sasa ya kuhakikisha Somalia inaondokana na utegemezi kwa kuibua mbinu za kujipatia kipato baada ya kutia saini ushirikiano na taasisi za fedha duniani ikiwemo IMF huku Benki ya Dunia na Umoja wa Mataifa wakiunga mkono.

(Sauti ya Michael Keating)

“Waziri Mkuu amekuwa makini sana katika hili na kwa kile tulichoshuhudia ndani ya miezi 18 ni ongezeko la mapato ya ndani kutokana na makusanyo ya kodi na ushuru na kuimarika kwa matumizi bora ya fedha za umma, mathalani askari wanalipwa mishahara kwa kutumia vitambulisho vya kisasa na wana akaunti za  benki na pia kuna mfumo wa kutathmini watumishi wa umma na malipo.”

Kuimarika kwa usalama nako ni miongoni mwa mafanikio amesema licha ya changamoto zilizopo pamoja na mchakato wa amani na maridhiano, ingawa amesema bado safari ni ndefu.

Hata hivyo amesema licha ya mafanikio  hayo vyombo vya habari vya kimataifa vimeipa kisogo Somalia katika  uandishi wa habari za mafanikio..

(Sauti ya Michael Keating)

“Havipo kwa kiasi  kikubwa nchini Somalia, na wanaonekana hawawezi kuja kwa sababu ya gharama ya bima labda kuwepo na habari kubwa na habari hizo kubwa ni zile zinazohusiana na njaa, ukame au ghasia, hii ikimaanisha iwapo jambo baya linatokea watu wengi wanaibuka kuandika na kutoweka na iwapo ukitafuta Somalia kwenye mtandao utaona ni habari mbaya tu. Lakini ukweli ni kwamba kuna mabadiliko,”