UNHCR yapongeza Ukrane kwa kupitisha pensheni ya wakimbizi wa ndani

11 Septemba 2018

Mahakama kuu zaidi nchini Ukraine imetoa uamuzi unaosaidia mamia kwa maelfu ya wazee, wakimbizi wa ndani na wakaazi katika maeneo yasiodhibitiwa na serikali kupata pensheni zao ambazo wamekosa  tangu 2014.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limefurahia uamuzi huo wa tarehe 4 Septemba ukisema  kama ni hatua muhimu katika kufuta machozi kwenye macho ya waathirika wa mgogoro wa miaka mitano nchini Ukraine ambao kwa sasa wako katika uhitaji mkubwa wa msaada.

Mkurugenzi wa UNHCR, Ulaya Pascale Moreau, akiipongeza Ukraine kwa hatua hiyo adhimu, amewaimba mamlaka ya nchini hiyo kuhakikisha kwamba uamuzi huo umetekelezwa haraka iwezekanavyo ili kutuliza nyoyo za watu wanaotegemea penshehi kupata mahitaji ya msingi.

Sasa ni miaka mitano mapigano yakiendelea kuibua madhila kwa maelfu ya watu mashariki mwa Ukraine.

Kwa mantiki hiyo, UNHCR imepaza tena sauti yake ikiiomba jamii ya kimataifa kuendeleza msaada kwa watu milioni 3.4 wanohitaji msaada wa kibinadamu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud