Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 150,000 wamefungasha virago Ukaine na idadi inaongezeka kila saa:UNHCR 

Masha binti wa miaka 9 mkimbizi kutoka Ukraine akiunda mchezo wa kompyuta darasani mjini Minsk Belarus ambyo ni sehemu ya programu za watoto eKIDS kupitia mradi unaofadhiliwa na shirika la UNHCR na EPAM System (Toka maktaba)
UNHCR/Egor Dubrovsky

Amani na Usalama

Idadi ya watu wanaofungasha virago na kukimbia Ukraine kwenda kusaka usalama nchi jitrani “sasa ni zaidi ya 150,000 na inatarajiwa kuongezeka zaidi kwa mujibu wa Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi.

Kupitia ujumbe wake wa Twitter mapema leo Grandi amesema “watu hao ambao wamevuka mpaka na kuingia nchi za jirani nusu yao wameingia Poland huku wengine wengi wakibisha hodi Hungary, Moldova, Romania na kwengineko.” 

Ameongeza kuwa mbali ya wanaovuka mpaka kwenda nje ya nchi widadi ya wale wanaotawanya ndani ya nchi inaongezeka kwa kasi lakini operesheni za kijeshi zinazoendelea zinafanya kuwa vigumu  kukadiria idadi kamili na kuwapa msaada. 

Amesisitiza kuwa “UNHCR na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na wadau wa misaada ya kibinadamu wanafanya kila liwezekanalo ili kuweza kuwafikishia msaada wa dharura maelfu ya watu walioathirika na mzozo unaoendelea nchini Ukraine.”