Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu milioni 4.4 wafungasha virago nchini Ukraine:UN 

Tarehe 5 Machi watoto na familia zikiwasili Berdyszcze, Poland baada ya kuvuka mpaka kutoka Ukraine wakikimbia machafuko yaliyoshika kasi
© UNICEF/Tom Remp
Tarehe 5 Machi watoto na familia zikiwasili Berdyszcze, Poland baada ya kuvuka mpaka kutoka Ukraine wakikimbia machafuko yaliyoshika kasi

Zaidi ya watu milioni 4.4 wafungasha virago nchini Ukraine:UN 

Msaada wa Kibinadamu

 Katika muda wa wiki mbili, zaidi ya watu milioni 4.4 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mapigano nchini Ukraine yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo. 

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, watu milioni 1.85 wamekimbia makazi yao ndani ya Ukraine na wengine zaidi ya milioni 2.5 wamevuka mipaka ya kimataifa ya Ukraine. 

Jumla ya watu wote walioathirika na mzozo huo wa Ukraine hadi sasa ni milioni 12.65 

Kwa upande wake ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu masuala ya Kibinadamu OCHA pia inaripoti kwamba maeneo makubwa ya ya wakimbizi wa ndani au IDP yapo magharibi na kaskazini magharibi mwa Ukraine.  

Maeneo hayo ni pamoja na Zakarpatska, yenye wakimbizi wa ndani zaidi ya 500,000, Lvivska  wakimbizi 387,000 na Volynska wakimbizi 170,000. 

"Watu waliotawanywa ambaomwengi ni wanawake, watoto na wazee  wanakabiliwa na hatari kubwa za ulinzi na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu wa aina mbalimbali kulingana na mahitaji yao maalum," OCHA imesema katika ripoti yake ya hivi karibuni ya hali ya kibinadamu nchini Ukraine iliyotolewa jana Machi 10, 2022. 

Mama raia wa Ukraine akimfariji mwanawe mwenye umri wa miaka 7 akingojea usafiri huko Isaccea, Romania
© UNICEF/Adrian Câtu
Mama raia wa Ukraine akimfariji mwanawe mwenye umri wa miaka 7 akingojea usafiri huko Isaccea, Romania

Poland inawahifadhi wakimbizi milioni 1.5 kati ya milioni 2.5 

Takriban watu milioni 2.5 wamevuka mipaka ya kimataifa, tangu Februari 24 na 116,000 kati yao ni raia wa nchi ya tatu. 

"Idadi ya wakimbizi kutoka Ukraine kwa kusikitisha sasa imefikia milioni 2.5. Pia tunakadiria kuwa karibu watu milioni mbili wamekimbia makazi yao Ukraine na kutawanywa ndani ya Ukraine,” Amesema mkuu wa UNHCR Filippo Grandi kupitia ukurasa wake wa Twitter. 

Ameongeza kuwa mamilioni ya watu wanalazimishwa kutoka makwao kwa sababu ya vita hivi vya kipumbavu.  

Kati ya zaidi ya watu milioni 2.5 ambao wamekimbia Ukraine, Poland ndiyo inayohifadhi idadi kubwa zaidi, ikiwa na wakimbizi milioni 1.52, wakiwemo karibu 90,000 waliowasili jana Alhamisi pekee amesema msemaji wa UNHCR Matthew Saltmarsh kwa njia ya video akizungumza na waandishi wa Habari akiwa karibu na mpaka wa Poland. 

Hata hivyo, huku takriban watu 200,000 wakiwa wamekimbilia nchi jirani katika muda wa saa 24 zilizopita, hesabu hii inaweza kuongezeka zaidi. 

Pia amesema inawezekana kwamba idadi ya watu milioni 4 inayotarajiwa ikiongezeka haitashangaza. 

Kulingana na mashirika ya kibinadamu, harakati hizi za watu kuvuka zingekuwa kubwa zaidi endapo mapigano na kuzingirwa kwa baadhi ya miji kusingezuia maelfu ya raia kukimbia ghasia.  

Hakika, kuchelewa kuwahamisha raia kutoka mji uliokumbwa na vita wa Mariupol kumeacha "mamia ya maelfu ya watu kukwama katika janga la kibinadamu linaozidi kuzorota". 

Watu zaidi la 500,000 wamesaidiwa Ukraine 

Huku kukiwa na jwimbi kali la majira ya baridi, shirika la afya duniani (WHO) linasema watu waliokimbia makazi yao wanakabiliwa na hatari zinazoongezeka za hypothermia, baridi kali, magonjwa ya kupumua na matatizo ya afya ya akili. 

Tarehe 5 Machi 2022 mashariki mwa Ukraine, watoto na familia wakielekea katika mpaka kuvuka kuingia Poland.
© UNICEF/Viktor Moskaliuk
Tarehe 5 Machi 2022 mashariki mwa Ukraine, watoto na familia wakielekea katika mpaka kuvuka kuingia Poland.

"Hali za sasa katika maeneo mbalimbali nchini humo zinafaa kwa mlipuko na kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza," limeonya shirika hilo la afya la Umoja wa Mataifa. 

Hivi sasa, mashirika ya kimataifa ya kibinadamu yanaongeza msaada wao katika changamoto kubwa ya kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu nchini Ukraine. Kwa hivyo Umoja wa Mataifa unasema mashirika hayo yanapeleka wafanyikazi wa ziada kote nchini na kujitahidi kusafirisha vifaa kwenye maghala katika vituo tofauti, nchini Ukraine na nje ya nchi. 

Hadi sasa, Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake wametoa msaada wa kibinadamu kwa zaidi ya watu 500,000 nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na chakula cha kuokoa maisha, malazi, blanketi na vifaa vya matibabu. 

Kwa upande wake, shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) linapanga kusaidia hadi watu milioni 3.1.  

Kipaumbele chake ni kusambaza chakula kingi katika miji ya Ukraineikiwemo , mikate na mgao wa chakula. Huku msaada wa chakula ukiwasili kila siku, WFP iko katika inakimbizana na muda wa kutayarisha chakula katika maeneo ambayo mapigano yanatarajiwa kuzuka.