Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za pamoja zitasaidia kupunguza visa vya kujiua duniani-WHO

Tiba muhimu zaidi kwa msongo wa mawazo ni mazungumzo. Picha: UM/Video capture

Juhudi za pamoja zitasaidia kupunguza visa vya kujiua duniani-WHO

Afya

Juhudi za pamoja zitasaidia kuongeza uelewa wa tatizo la kujiua na hivyo kunusuru maisha ya watu wengi , limesema leo shirika la afya  duniani WHO . Flora Nducha taarifa kamili

Wito huo umetolewa leo kwa ushirikiano na chama cha kimataifa cha kuzuia kujiua (IASP) katika kuadhimisha siku ya kuzuia vitendo vya kujiua duniani ambayo kila mwaka huwa tarehe 10 Septemba.

Kusudi la siku hii ni kuongeza uelewa duniani kote kuwa kujiua kunaweza kuzuiwa. Profesa Murad Khan ni Rais wa Chama cha kimataifa cha kuzuia kujiua anaifafanua kauli mbiu ya mwaka huu inayosema, ‘Kufanya kazi pamoja ili kuzuia kujiua’

(SAUTI YA MURAD KHAN)

"Mada hii inaonyesha kipengele muhimu cha kuilinda jamii kwa ufanisi ambacho ni ushirikiano. Hakuna shirika moja, au mtu mmoja mmoja mmojaa anaweza kutatua tatizo hili gumu la kujiua. Sababu mbalimbali za kujiua zinaleta changamoto kwetu sote "

Takwimu  za WHO zinaonesha kila mwaka takribani watu milioni moja hupoteza maisha kwa kujiua. Hii ni sawa na kuwa mtu mmoja hujiua kila sekunde 40. Idadi ya vifo vya kujiua inazidi idadi ya vifo vinavyotokana na mauaji ya kawaida na vita kwa pamoja.

Profesa Murad Khan anatoa wito kwa jamii nzima kushiriki kulitatua taizo hili ambalo

 (SAUTI YA MURAD KHAN)

“Mwaka huu tunatoa wito kwako kama mwanafamilia, mwanajamii, wataalam wa afya, kumwangalia jirani yako na kufikiri ni kwa namna gani unaweza kushiriki na kufanya kazi kwa pamoja kueleza changamoto za kujiua katika eneo lako, Jamii yako nan chi yako”

Miaka iliyopita, shughuli zaidi ya 300 za kuiadhimisha siku hii zilifanyika katika nchi takribani 70 ikiwa ni pamoja na matukio ya kuelimisha, mikutano na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya Facebook na Twitter.