Uganda imezindua chanjo ya kipindupindu ikiwalenga watoto milioni 1.6-WHO

6 Septemba 2018

Uganda imeanza kampeini kubwa ya chanjo ya matone dhidi ya kipindupindu na inalenga watu zaidi ya milioni moja katika maeneo 11 ambako kunazuma mlipuko wa ugonjwa huo mara kwa mara. 

Walengwa hasanwa kampeni hiyo kwa mujibu wa shirika la afya  ulimwenguni, WHO, ni watoto wa umri kati ya  mwaka mmoja hadi miaka 15 ingawa serikali ya Uganda inasema na watu wazima watashirikishwa katika chanjo hiyo.

Sarah Opendi ni waziri wa Afya wa masuala ya jumla  ya afya nchini Uganda anafafanua sababu za uzinduzi wa chanjo hiyo, akisema ni kutokana na kila mwaka milipuko hutokea katika sehemu mbalimbali.

Na kwa nini ni muhimu pia kutoa chanjo hiyo kwa watu wazima? asem ani kwa sababu  wakati ugonjwa huo unapotokea pia huwaathiri watu wote kwa sababu hamna vyoo. 

Wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika kaskazini magharibi mwa nchi hiyo waziri mwenza wa afya  Dkt Jane Ruth Aceng amesema kila mwaka hutokea wastani wa visa vya kipindupindu 1,850 na vifoni 45 na vingi hutokea katika wilaya za Mashariki, Kaskazini na Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.  Na kampeini imefadhiliwa na  shirika la kimataifa la muungano wa chanjo ,GAVI na dawa hiyo yam atone ndio inatumika kwa mara ya kwanza nchini Uganda.

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud