Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa amesema amefarijika na hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo kupiga kura na kupitisha azimio la kutaka pande zote katika mizozo kusitisha uhasama ili kutoa fursa ya kutoa chanjo dhidi ya corona au Covid-19 na misaada mingine ya kibinadamu.
Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamezikosoa nchi zinazojaribu kubinafsisha na kuhodhi chanjo yoyote ya dhidi ya corona au COVID-19 inayotarajiwa kupatikana wakisema njia pekee ya kupambana na janga hili ni kuhakikisha chanjo inapatikana kwa gharama nafuu kwa kila mtu duniani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameuambia mkutano wa kimataifa kuhusu chanjo unaofanyika leo kupitia njia ya mtandao kwamba chanjo ni muhimu sana na imeokoa maisha ya mamilioni ya watu duniani lakini peke yake haitoshi kukabiliana na majanga makubwa ya kiafya kama linaloisumbua dunia hivi sasa la COVID-19.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO amesema kwa muda mrefu Marekani imekuwa mshirika mkubwa wa WHO na anatimai kwamba itaendelea kuwa hivyo.
Kutokana na taarifa iliyotolewa hii leo mjini Atlanta na New York Marekani, pamoja na Geneva Uswisi, wakati COVID-19 ikizidi kusambaa duniani, zaidi ya watoto milioni 117 katika nchi 37 wanaweza kukosa kupokea chanjo ya kuokoa maisha dhidi ya surua.
Kutokana na taarifa iliyotolewa hii leo mjini Atlanta na New York Marekani, pamoja na Geneva Uswisi, wakati COVID-19 ikizidi kusambaa duniani, zaidi ya watoto milioni 117 katika nchi 37 wanaweza kukosa kupokea chanjo ya kuokoa maisha dhidi ya surua.
Ugonjwa unaozuilika wa kichomi unakatili maisha ya watoto wengi kuliko maradhi mengine yoyote kwa mujibu wa taarifa ya utafiti mpya iliyotolewa leo na mashirika matano ya kimataifa yanayohusika na masuala ya watoto likiwemo la Umoja wa Mataifa la UNICEF.