Watu milioni 1.4 kupewa chanjo dhidi ya kipindupindu Harare: WHO

3 Oktoba 2018

Serikali ya Zimbabwe pamoja na wadau wake likiwemo shirika la afya duniani WHO leo wamezindua kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu, OCV inayolenga watu milioni 1.4 kwenye mji mkuu Harare.

Taarifa ya WHO iliyotolewa leo mjini Harare inasema kampeni hiyo ya chanjo ni sehemu ya juhudi za kudhibiti mlipuko wa kipindupindu ulioripotiwa tarehe 6 mwezi uliopita wa Septemba na kwamba chanjo hiyo imetolewa na ubia wa chanjo duniani, GAVI, ubia ambao pia unagharimia kampeni nzima.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika, Dkt Matshidiso Moeti, amesema kuwa mlipuko wa sasaumejikita zaidi katika viunga vya Harare ambako kuna idadi kubwa ya watu, lakini kuna fursa ya kukabiliana nao kupitia chanjo hiyo ili kuepuka ugonjwa huo kuenea zaidi kwenye maeneo mengine ambako itakuwa vigumu kuudhibiti.

Mbali na chanjo , serikali ikisaidiwa na WHO imeweka mikakati mingine ya udhibiti kama vile utoaji wa maji safi, na kuhimiza usafi, kusafisha mitaro ya na pia kuweka vituo  kadhaa vya matibabu.

Chanjo dhidi ya kipindupindu itakuwa ya awamu mbili ikitilia mkazo  mitaa ya Harare na Chitungwiza ulioko umbali wa kilomira 30 kusini mashariki mwa mji mkuu  ambayo iliathirika mno na mlipuko huu .

WHO inasema ili kuepusha usugu wa muda mrefu kwa wananchi, dozi ya pili itatolewa katika maeneo yote wakati wa duru ya pili ya chanjo hapo baadaye.

Afisa Mtendaji Mkuu wa GAVI Dkt Seth Berkley, amesema kuwa kipindupindu ni ugonjwa ambao unaweza kuzuilika kwa kutumia maji safi pamoja na kuzingatia usafi na kuongeza kuwa hakuna sababu kwanini watu wawe wanaendelea kufa kutokana na ugonjwa huu mbaya.

Wafanyakazi wa huduma za afya pamoja na Madakatari wa shirika la MSF wamuhudumia mama mmoja katika zahanati ya kutibu Kipindupindu mjini Chegutu Zimabbwe mwaka 2008.
© UNICEF/Christine Nesbitt
Wafanyakazi wa huduma za afya pamoja na Madakatari wa shirika la MSF wamuhudumia mama mmoja katika zahanati ya kutibu Kipindupindu mjini Chegutu Zimabbwe mwaka 2008.

 

Pia amesema kuwa GAVI imefanya juhudi kubwa  kuona kama dawa ya chanjo dhidi ya kipindupindu huwa iko tayari wakati wowote ili kusaidia  kukabilina na milipuko kama huo.

Kipindupindu kimekuwa kikitokea kila mara nchini Zimbabwe ambapo mlipuko mkubwa  ulitokea Agosti 2008 hadi Mei 2009 na kuwaua watu zaidi ya 4000.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter