Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hisani si lazima , lakini thamani yake katika jamii ni kubwa:UN

Jamii wanaoishi na umaskini Sonagachi, Kolkata, India.(Picha:UM/Kibae Park)

Hisani si lazima , lakini thamani yake katika jamii ni kubwa:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Hisani, kama mawazo ya kujitolea na uhamasishaji wa kusaidia wengine, huleta uhusiano wa kweli wa kijamii na huchangia kuundwa kwa jamii imara zaidi.

Siku ya Kimataifa ya hisani ilianzishwa kwa lengo la kufahamisha na kuhamasisha watu, mashirika yasiyo ya serikali, na wadau duniani kote ili kuwasaidia wengine kupitia shughuli za kujitolea ufadhili au hisani. Tarehe ya 5 Septemba ilichaguliwa kuadhimisha siku hii kila mwaka ili kuadhimisha kumbukumbu ya kufa kwa Mama Teresa wa Calcutta, ambaye alipokea tuzo ya amani ya Nobel mwaka wa 1979 "kwa ajili ya kazi ializozifanya  katika jitihada za kuushinda umaskini na dhiki, ambayo pia ni tishio kubwa kwa amani. "

Katika agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu iliyopitishwa Septemba 2015, Umoja wa Mataifa unatambua kwamba kutokomeza umasikini katika aina na viwango vyake vyote, ikiwa ni pamoja na ufukara ni changamoto kubwa zaidi duniani na ni mahitaji ya lazima kwa maendeleo endelevu. Agenda hiyo pia inataka moyo wa kuimarisha mshikamano wa kimataifa, hususani katika mahitaji ya watu masikini zaidi na walioko katika mazingira hatarishi.

 

Image
Bado umaskini uliokithiri unaendelea kwenye baadhi ya maeneo duniani kote, kama hapa Darfur, nchini Sudan. Picha ya UN/Albert González Farran

Inatambua jukumu la sekta binafsi, kuanzia makampuni madogo hadi vyama vya ushirika, kwa mashirika ya kimataifa, na yale ya kiraia pia mashirika ya misaada katika utekelezaji wa agendahiyo mpya.

Umoja wa Mataifa unasema malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yaliyowekwa katika agenda yanaweza kugawanywa katika maeneo sita muhimu: watu, sayari, ustawi, amani, na ushirikiano.

Malengo haya yana uwezo wa kubadilisha maisha yetu na sayari yetu kwa kutoa mfumo unaohitajika kwa taasisi za hisani ili kuwawezesha watu wote kuchangia katika uboreshaji wa dunia yetu.