Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mandhari ya mto Tarangire yaibuka kidedea shindano la picha GLF

Mto Tarangire kama unavyoonekana kutoka bunga la Tarangire Arusha, Tanzaniaambapo shughuli za kibinadamu zinatishia uwepo wa mto huo.
Lameck Kiula/GLF Nairobi 2018
Mto Tarangire kama unavyoonekana kutoka bunga la Tarangire Arusha, Tanzaniaambapo shughuli za kibinadamu zinatishia uwepo wa mto huo.

Mandhari ya mto Tarangire yaibuka kidedea shindano la picha GLF

Tabianchi na mazingira

Jukwaa la kimataifa la kurejesha ubora wa misitu, kuzuia mmomonyoko wa udongo na kutoa fursa za maendeleo barani Afrika GLF 2018,  linaendelea mjini Nairobi nchini Kenya, likiambatana na matukio mbalimbali ya kuonyesha jitihada zinazofanywa na mataifa ya Afrika kulinda ardhi na misitu inayolizunguka.

Moja ya matukio yaliyovutia wengi ni kutangazwa kwa washindi wa mashindano ya picha ya GLF Nairobi 2018. Kwa mujibu wa waandaji wa jukwaa hilo GLF na kituo cha kimataifa cha utafiti wa misitu CIFOR, picha zaidi ya 400 kutoka kote barani Afrika zenye ubora wa aina yake zikionyesha tofauti, ubunifu na hamasa ziliwasilishwa na kuingizwa katika shindano hilo .

Kwa pamoja picha hizo zimeonyesha uzuri wa ardhi na mandhari ya bara la Afrika na juhudi zinazofanyika mashinani kuhakikisha uzuri huo unalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, mmomonyoko wa udongo na kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanatimia ifikapo 2030.

 

Uzuri wa  mandhari ya mchanga uliojipanga mithili ya mchoro katika jangwa la Namib ujulikanao kama Namib Rand dune
Phil Sturgess/GLF Nairobi 2018
Uzuri wa mandhari ya mchanga uliojipanga mithili ya mchoro katika jangwa la Namib ujulikanao kama Namib Rand dune

Baada ya picha hizo kuwekwa kwenye wavuti wa GLF watu walipata fursa ya kupiga kura kuchagua washindi. Na hatimaye washindi wamepatikana ambao GLF inasema wamestahili. Nafasi ya kwanza ya mshindi wa jumla ikaenda kwa picha ya  mandhari ya mto Tarangire uliopo kwenye hifadhi ya mbuga ya Wanyama ya Tarangire mkoani Arusha nchini Tanzania, picha hiyo iliwasilina na Lameck Kiula.

Mshindi wa pili ni picha inayoonyesha uzuri wa  mandhari ya mchanga uliojipanga mithili ya mchoro katika jangwa la Namib ujulikanao kama Namib Rand dune,  ambayo iliwasilishwa na Phil Sturgess.

Kaskazini mwa Rwanda-Karongi eneo ambalo lilikuwa hatari kwa watu baada ya wao kuhama eneo hili sasa ni mlima wa mimea ya kijani.
Elie NTIRENGANYA/GLF Nairobi 2018
Kaskazini mwa Rwanda-Karongi eneo ambalo lilikuwa hatari kwa watu baada ya wao kuhama eneo hili sasa ni mlima wa mimea ya kijani.

Na Ushindi wa tatu ukanyakuliwa na picha ya mandhari ya muinuko wa mlima Umuganda wa nchini Rwanda iliyoingizwa shindanoni na Elie Ntirenganya.

Lakini pia kuliwa na picha ambazo zilipata kura nyingi japo sio washindi kama vilepicha  iliyoonyesha mmea wa bahati ndani ya mapango ya Amboni yaliyoko mkoani tanga nchini Tanzania iliyowasilishwa na Peter Masinde.

TAGS: GLF, Afrika, shindano la picha, Nairobi, tarangire, Umuganda,