Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ni lazima ibadilike sanjari na mabadiliko ya tabia nchi:GLF

Misitu inatoweka
World Bank/Curt Carnemark
Misitu inatoweka

Afrika ni lazima ibadilike sanjari na mabadiliko ya tabia nchi:GLF

Tabianchi na mazingira

Bara la Afrika limetakiwa kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na mmomonyoko wa udongo ukaotokana na sababu mbalimbali , ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi ili kunusuru misitu, uhakika wa chakula, ajira na maendeleo katika bara hilo kwa mujibu wa jukwaa la kimataifa la kurejesha ubora wa ardhi matarajio na fursa barani Afrika ( GLF) 2018 lililoanza leo mjini Nairobi nchini Kenya  . 

Afisa wa serikali ya Kenya ambao ndio wenyeji wa mkutano huo akitangaza kuanza rasmi kwa jukwaa hilo mjini Nairobi, lililowaleta pamoja zaidi ya washiriki 800 kutoka serikali, sekta za fedha, sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia, watu wa jamii za asili, wanasayansi, mashirika yasiyo ya kiserikali na vijana kujadili jinsi gani ya kurejesha ubora wa ardhi barani Afrika.

Inakadiriwa kwamba ekari bilioni 2.8 za misitu hupotea kila mwaka , huku ukataji miti na mmomonyoko wa udongo vikisalia kuwa changamoto kubwa barani Afrika.

Mkutano huo una lengo la kuonyesha mafanikio, changamoto na msaada wa kisiasa na kijamii katika utekelezaji wa mradi wa Afrika wa kurejesha ubora wa ekari milioni 100 za ardhi iliyoathirika na mmomonyoko wa udongo AFR 100, barani humo ifikapo mwaka 2030 pia kuhakikisha kuna kuwa na mikakati endelevu itakayohusisha sekta mbalimbali na wadau wote kupata njia muafaka za kutimiza lengo hilo, nani ashirikishwe na kwa njia gani.

 Dr Robert Nasi, mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa misitu CIFOR ambao ni miongoni mwa waandaji wa jukwaa hilo nae anahudhuria .Na sasa mambo yamebadilika 

Hivyo ni wajibu wa bara la Afrika kuchukua hatua. Naye mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP Erik Solheim akisisitiza umuhimu wa mchakato wa kuboresha tena ardhi amesema, “ ni bayana kwamba kuna vuguvugu kubwa linaloongezeka la kurejesha ardhi katika ubora na washirika wetu wote wa kimataifa katika nyanja hii wanaafiki kwamba wakati wa kuongeza juhudi ni sasa kwani kuna uwezekano mkubwa wa kuokoa ekari milioni 350 zilizoathirika na mmomonyoko duniani ifikapo 2030, kitu ambacho kitapiga jeki kwa kiasi kikubwa hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, kupotea kwa bayoanuai na kupambana na umasikini kwani zaidi ya asilimia 70 ya watu wa Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara, wanategemea misitu kwa ajili ya kuishi.

Jukwaa hilo la siku mbili litamazilika kesho Alhamisi limeanadaliwa na CIFOR kwa ushirikiano na UNEP, Benki ya Dunia, GLF na wadau wengine wa mazingira.