Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada watakiwa kuitikia mahitaji ya wakimbizi na wahamiaji wa Venezuela: UNHCR, IOM

Mamia ya raia wa Venezuela wakiwa wamepanga foleni kwenye kituo cha usaidizi cha mpakani wakisubiri kuingia Peru kupitia mpaka wa Ecuador. Misururu kama hii inaweza kumchukua mtu hadi saa 10 kuweza kuruhusiwa kupita.
UNHCR/Sebastian Castañeda
Mamia ya raia wa Venezuela wakiwa wamepanga foleni kwenye kituo cha usaidizi cha mpakani wakisubiri kuingia Peru kupitia mpaka wa Ecuador. Misururu kama hii inaweza kumchukua mtu hadi saa 10 kuweza kuruhusiwa kupita.

Msaada watakiwa kuitikia mahitaji ya wakimbizi na wahamiaji wa Venezuela: UNHCR, IOM

Msaada wa Kibinadamu

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na lile la uhamiaji, IOM,  wametoa wito wa pamoja kwa jamii ya kimataifa kutoa misaada zaidi ili kuitikia mahitaji ya wakimbizi na wahamiaji wa Venezuela katika nchi mbali mbali za ukanda wa Amerika Kusini.

Kamishina Mkuu wa UNHCR, Fillipo  Grandi amesema hii inetokana na ongezeko la idadi ya wavenezuela wanaokimbilia au kuhamia nchi mbalimbali katika ukanda huo.

Bwana Grandi amezipongeza nchi zinazpkubali kupokea wakimbizi na wahamiaji hao licha ya changamoto zinazoambatana na kuwahifadhi, lakini pia ameonyesha kusikitishwa na mabadiliko ya sera ya hivi karibuni nchini Ecuador na Peru yanayoathiri wakimbizi na wahamiaji, mfano ukiwa ni vikwazo vya kupata kibali cha kuingia nchi hizo na hati ya kusafiri.

Akiongeza sauti yake kuomba msaada wa kibinadamu kwa ajili wavenezuela, Mkurugenzi Mkuu wa IOM, William Lacy Swing, ameomba ushirikiano zaidi na nchi zinazowahifahdi

 Amesema msaada unahitajika ili kukabiliana na changamoto ya kifedha inayoathiri shughuli zao kwa watoto waliotengaga na familia zao na kukimbia bila kusindikizwa na mtu mzima yeyote na sasa wakikabiliwa na hatari ya kutopatiwa vyeti vya makazi au usafiri.

Hali hii inatumbukiza watoto katika hatari ya unyonyaji, usafirishaji haramu na ukatili, amesema Mkurugenzi Mkuu huyo wa IOM.

Inakadiriwa kuwa Wavenezuela milioni 3.9 wanishi nje ya nchi yao wakiwemo milioni 1.6 waliolazimika kutoroka mzozo nchini mwao tangu mwaka wa 2015.