Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

 Idadi ya wakimbizi na wahamiaji wa Venezulea yafikia milioni 3

Wakimbizi wa Venezuela wakiwasili Manaus, Brazil
César Nogueira/ Acnur Brasil
Wakimbizi wa Venezuela wakiwasili Manaus, Brazil

 Idadi ya wakimbizi na wahamiaji wa Venezulea yafikia milioni 3

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na lile la uhamiaji, IOM, yametangaza leo kwamba idadi ya wakimbizi na wahamiaji kutoka Venezuela sasa imefikia milioni 3. Grace Kaneiya na taarifa kamili

Kwa mujibu wa mashirika hayo takwimu zilizotolewa na mamlaka ya kitaifa ya uhamiaji  na ofisi zingine husika, nchi za Amerika ya Kusini  na Caribbea zinahifadhi takribani wakimbizi na wahamiaji milioni 2.4 kutoka Venezuela huku waliosalia wako katika nchi zingine duniani.

Mwakilishi wa pamoja wa IOM na UNHCR kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji kutokja Venezuela Eduardo Stein amezipongeza nchi hizo za Amerika ya Kusini na Caribea kwa kuacha milango yao wazi kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji hao kutoka Venezuela, hata hivyo amesema vituo vyao vya mapokezi vimefurika na vinahitaji msaada wa haraka na hatua kutoka jumuiya ya kimataifa endao ukarimu huo utaendelea.

Colombia ndio ina idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji kutoka Venezuela wakiwa ni Zaidi ya milioni moja , ikifuatiwa na Peru zaidi ya laki 5, Ecuador zaidi ya laki 2, Argentina 130,000, Cile zaidi ya laki moja na Brazil 85,000.