Ukame waongeza machungu kwa wananchi Afghanistan

15 Agosti 2018

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema mzozo unaoendelea nchini Afghanistan, majanga ya asili, ukimbizi wa ndani vinaendelea kusababisha ongezeko la ukosefu wa uhakika wa chakula nchini humo.

Likinukuliwa na wavuti inayochapisha habari za usaidizi wa kibinadamu, RELIEF WEBFAO inasema kama majanga hayo hayatoshi, mwaka huu ukame ambao umekumba eneo kubwa la nchi hiyo nao umeathiri wakulima.

Miongoni mwao ni Ahmadullah mkulima mdogo anayemiliki mifugo na analima matunda kwenye eneo dogo la shamba lake.

Ukame umesababisha bustani zake kukauka na mazao mengi  yamedhoofika. Wanyama hawazai tena na alilazimika kuwauza wote. Yeye na majirani zake wote wanakumbwa na hali hiyo. Hawawezi kununua chakula cha mifugo kutokana na kwamba bei zimepanda kwasababu ya ukame,” imesema taarifa hiyo na kwamba chaguo pekee ni kuuza nyama kwa bei ya chini.

 “Tangu wakati wataliban wanatawala, mara nyingi nimekuwa nikikopa fedha kutoka kwa jamaa na marafiki ili kupata chakula cha kutosha," amesema Ahmadullah na kuongeza kuwa "nina wasiwasi itakuwa hivyo hivyo mwaka huu, au mbaya zaidi  mwaka huu. Itabidi tuhame. Lakini kwa kuwa majimbo mengi yanakabiliwa na ukame, sijui tutakwenda wapi.

Katika kubabiliana na tatizo hilo wafugaji wengi wamebuni mbinu ya kuchimba visima vya kwa ajili ya maji ya kunywa na umwagiliaji, mkakati ambao hata hivyo si endelevu.

FOA kupitia miradi yake kupunguza makali ya ukame jimboni Kandahar,  imewapatia Abdullah na majirani zake mgao wa chakula cha mifugo kwa sababu kutokana na  ukame wa mara kwa mara, wakulima hawana muda wa kuijikwamua na hali  hiyo .

Kandahar ni moja ya majimbo yaliyoathiriwa zaidi na ukame nchini Afghanistan.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter