Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Apu mpya yasaidia wakimbizi tafsiri ya lugha za kigeni

Picha: IOM
Apu mahsusi kwa ajili ya wahamiaji.

Apu mpya yasaidia wakimbizi tafsiri ya lugha za kigeni

Wahamiaji na Wakimbizi

Apu mpya iliyobuniwa na wanafunzi wawili wa Chuo kimoja kikuu cha nchini Marekani imesaidia wakimbizi kuondokana na tatizo la lugha pindi wanapofika ugenini.

Ikipatiwa jina la Tarjimly, apu hiyo imebuniwa na Atif Javed na Aziz Alghunaim, wanafunzi wataasisi ya teknolojia ya Massachussets, MIT ya nchini Marekani mbapo Atif anaeleza..

“Tarjimly ni apu inawasaidia wakimbizi na watoa misaada kuwasiliana kwa kuwaunganisha pamoja na mtu wa kutafsiri lugha kwa kujitolea katika kipindi cha sekunde 60 tu. Wanaweza kuwasiliana kwa kutuma nyaraka, ujumbe mfupi wa simu, au kuzungumza kwa simu wakionana.”

Atif anasema bibi yake ambaye alitoka India aliwasili Marekani akiwa mkimbizi lakini angalau yeye aliweza kumsaidia kutafsiri lugha lakini wengi mamilioni huteseka.

“Fikiria ikiwa huwezi kuzungumza na wakili wako ama daktari mambo yanakuwa magumu.”

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema hadi sasa zaidi ya watu 3,000 wamejitolea kusaidia kutafsiri.