Skip to main content

Chuja:

tafsiri

UN News

Kiswahili kinalipa-mwanafunzi chuo kikuu cha Nairobi, Kenya

Kiswahili kinazidi kutamba na kutambuliwa kama lugha muhimu hata katika mafunzo ya tafsiri na ukalimani hususan nchini Kenya, katika Makala ya wiki hii Grace Kaneiya  wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amevinjari katika chuo kikuu cha Nairobi kitengo cha tafsiri na ukalimani ambapo amezungumza na mhadhiri katika kitengo hicho vile vile wanafunzi. Kulikoni basi nakupeleka moja kwa moja hadi Nairobi, Kenya.

Sauti
5'53"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki- Fasili, Fasiri, Tafsiri

Katika neno la wiki hii leo, Bi. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA anachambua tofauti za maneno Fasili, Fasiri na Tafsiri. Anasema ni maneno aina ya nomino na yana maana tofauti kabisa. Fasili ni pale  unaelezea maana ya neno kwa lugha  yake asili, ilhali fasiri ni pale unapolitaja kwa lugha ya  kigeni. Tafsiri ni neno linapoelezewa maana yake kwa lugha nyingine lakini katika maandishi ambapo kwa maneno itakuwa ukalimani.

Sauti
1'3"
UN News/Assumpta Massoi

Kazi yetu ni muhimu lakini mara nyingi haijulikani- Mfasiri

Tafsiri kutoka lugha moja  hadi nyingine imekuwa ina mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Umoja wa Mataifa, amesema Lydie Mpambara, mmoja wa wafasiri wa lugha kwenye idara ya Baraza Kuu na mikutano  ya Umoja huo, DGACM.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ikiwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya tafsiri ya lugha duniani iliyoadhimishwa hivi karibuni, Bi. Mpambara ambaye anazungumza kiingereza, kifaransa, Kiswahili na kispanyola amefafanua jinsi kazi yao inavyochagiza majukumu ya Umoja wa Mataifa.

Sauti
2'23"