Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkondo joto kuendelea kutesa Ulaya- WMO

Mtoto akicheza kwenye maji wakati wa msimu wa joto kali
WMO
Mtoto akicheza kwenye maji wakati wa msimu wa joto kali

Mkondo joto kuendelea kutesa Ulaya- WMO

Tabianchi na mazingira

Mkondo joto uliopiga eneo la Ulaya magharibi mwanzoni mwa mwezi huu sasa  unaelekea Ulaya kaskazini. Shirika la hali ya hewa duniani, WMO limesema mkondo joto huo ulisababisha viwango vya juu zaidi vya joto kuwahi kufikiwa huko Ureno na Hispania katika kipindi cha miaka 37.

Msemaji wa WHO huko Geneva, Uswisi Sylvie Castongay amewaambia waandishi wa habari kuwa mji mkuu wa Ureno ulivunja rekodi na kufikia nyuzi joto 44 katika kipimo cha selsiyasi.

Amezungumzia pia maeneo ya Amerika ya Kaskazini akitolea mfano California akisema kiwango cha joto si cha kawaida na kwamba hali hiyo pamoja na ukame ndio vinazidi kuchochea moto wa nyikani ambao unazidi kukumba jimbo hilo.

Akifafanua kuhusu joto linaloongezeka kila uchao ikiwemo maeneo ya ncha ya kaskazini mwa dunia ambako awali theluji katu haikuwa inayeyuka kwa kwango cha sasa, mtaalamu wa mabadiliko ya hali ya hewa WMO Michael Sparrow amesema..

(Sauti ya Michael Sparrow)

“Ongezeko la joto tunaloshuhudia sasa na kumekuwepo na uchambuzi wa wanasayansi, inaonyesha kuwa mkondo joto wa sasa uko maradufu kutokana na mabadiiko ya tabianchi kuliko ilivyokuwa kabla ya zama za ukuaji wa viwanda.”