Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zikipamba moto Gaza, Guterres azidi kutiwa hofu 

Picha ya upande wa Palestina wa Karem Shalom ambako bidhaa zinaingia na kutoka kati ya Israel na Gaza , ambapo sehemu iliteketezwa kwa moto na Wapalestina, na kuathiri uwezo wake wa kusafirisha baadhi ya bidhaa cha chakula ikiwemo pia mafuta ya dharura. 1
Picha na UN

Amani na Usalama

Nina wasiwasi mkubwa juu ya ongezeko la ghasia huko ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati huu ambapo ghasia hizo zimesababisha vifo vya watu na majeruhi.

Vyombo vya habari Mashariki ya Kati vinaripoti kuwa jana ijumaa ni mara ya pili kwa vikosi vya Israel kukabiliana na kikundi cha Hamas na wanamgambo wa kipalestina kwenye uzio huo ambao umewekwa na Israel.

Kupitia msemaji wake, Katibu Mkuu amesema ni jambo jema pande zote kinzani kwenye mzozo huo ziondokane na hatari inayoweza kufanya mzozo huo kuwa mkubwa zaidi.

Ametoa wito kwa wafuasi wa kikundi cha Hamas na wanamgambo wa kipalestina waache kurusha maroketi na vishada vya moto kwenye eneo lenye uzio uliowekwa na Israel.

Halikadhalika ametoa wito kwa Israel ijizuie na kuepuka kuchochea zaidi mzozo huo kati yake na Palestina.
Bwana Guterres amesihi pande zote hizo zishirikiane na Umoja wa Mataifa hususan mratibu wake maalum na kufanya kazi ili kuondokana na hali ya hatari inayoendelea hivi sasa.

“Kuendelea kwa aina yoyote kwa hali ya sasa kutahatarisha maisha ya wapalestina na waisraeli, na kuongeza zaidi janga la kibinadamu kwenye ukanda wa Gaza. Na pia utadumaza juhudi za sasa za kuimarisha maisha ya wakazi wake na usaidizi wa kurejea kwa mamlaka ya Palestina Gaza,” amehitimisha Bwana Guterres.