Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunapomuenzi Mandelea tuenzi kwa vitendo aliyoyakumbatia:UN

Stempu iliotolewa na mamlaka ya posta ya Umoja wa Mataifa Julai 18, siku ya Mandela: Mchoraji Martin Mörck (Norway). muundaji: Rorie Katz (Umoja wa Mataifa)
United Nations Postal Administration (UNPA)
Stempu iliotolewa na mamlaka ya posta ya Umoja wa Mataifa Julai 18, siku ya Mandela: Mchoraji Martin Mörck (Norway). muundaji: Rorie Katz (Umoja wa Mataifa)

Tunapomuenzi Mandelea tuenzi kwa vitendo aliyoyakumbatia:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Nelson Mandelea alikuwa mtu wa vitendo na sio maneno matupu, tunapomuenzi tufanye hivyo kwa vitendo. Wito huo umetolewa hii leo kwenye na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye tukio maalumu la kumbukizi ya Mandela ambae angekuwa hai hii leo angekuwa na umri wa miaka 100 .

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na nchi wanachama na watu mbalimbali mashuhuri , mashirika ya Umoja wa Mataifa na waziri wa mazingira wa Afrika  Kusini kwa niaba ya taifa hilo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New york Marekani, Guterres amesema Mandela alikuwa shujaa, mwenye busara , mtu wa watu na aliyetekeleza alichosema kwani ni "Watu wachache sana katika historia wamekuwa na fikra za ulimwengu kama alivyofanya. Na wachache zaidi wameweza kutoa msukumo kama huo. Leo hii anasimama kama muhimuli wa maadili ya ulimwengu - amani, msamaha, unyenyekevu, uaminifu, hamasa, heshima na huduma. Madiba alituonyesha kuwa haya si maneno tu au ndoto bali ni hatua halisi ambazo wote tunaweza kuchukua."

 

Nelson Mandela alihutubia Baraza Kuu la Umoja waMataifa kama rais wa Afrika Kusini Oktoba  1995
UN Photo/G Kinch
Nelson Mandela alihutubia Baraza Kuu la Umoja waMataifa kama rais wa Afrika Kusini Oktoba 1995

Ametoa wito kuwa leo na kila siku ya kumuenzi Mandela watu wote duniani walete mabadiliko kwani Madiba "Alielewa kwamba sote tuna uwezo mikononi mwetu wa kuifanya dunia kuwa bora, dunia ambayo watu wanatendewa haki na usawa, bila kujali rangi, dini au jinsia , na kujenga dunia bora ni kazi na wajibu wa shirika letu.”

Ameongeza kuwa tumetoka mbali lakini bado tuna safari ndefu, lakini bahati nzuri kuna mkakati wa ajenda ya maendeleo endelevu wa 2030 ambao unaahidi kumaliza mifumo yote ya umasikini na kutomuacha yeyote nyuma akimnukuu Mandela"Kuondokana na umasikini sio ishara ya hisani ni kitendo cha haki. Ni kulinda misingi ya haki za kibinadamu, haki ya utu na maisha bora.Wakati umaskini unaendelea, hakuna uhuru wa kweli .” Mwisho wa kunukuu.

 

Mjumbe maalumu wa UNESCO kwa ajili ya amani na maridhiano na pia mchagizaji wa wa kimataifa wa SDGs, Forest Whitaker, akihutubia hadhira iliyokusanyika katika siku ya kimataifa ya Nelson Mandela
UN Photo/Rick Bajornas)
Mjumbe maalumu wa UNESCO kwa ajili ya amani na maridhiano na pia mchagizaji wa wa kimataifa wa SDGs, Forest Whitaker, akihutubia hadhira iliyokusanyika katika siku ya kimataifa ya Nelson Mandela

Kisha mzungumzaji mkuu katika tukio hilo akapanda jukwaani, Forest Whitaker mchagizaji wa malengo ya maendeleo endelevu na mwakilishi maalumu wa shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi, elimu na utamaduni UNESCO kwa ajili ya amani na maridhiano , na kusema Madiba alikuwa mtu wa kipekee

“Uwezo wake wa kukabiliana na maadui bila chuki ndicho kinachofanya maisha ya Mandela kuwa mfano halisi wa ubinadamu. Alielewa amani inaanzia moyoni na kama unataka amani ni lazima uwe na maridhiano na nafsi yako kwanza na kupitia elimu hiyo utatambua na kuleta mabadiliko duniani.”

Naye Edna Molewa waziri wa mazingira na wa Afrika Kusini nyumbani alikotoka Mandela akiliwakilisha taifa lake katika kumbukizi hiyo akakumbusha kwamba kama alivyokuwa Madiba kila binadamu ana mchango katika dunia hii. "Nelson Mandela aliamini kwamba , sote bila kujali ni kina nani tunaweza kuleta mabadiliko, aliamini kwamba kila mwanaume kila mwanamke na kila mtoto lazima wachukue jukumu la kuleta mabadiliko ya kuwa na dunia bora.”

 

Waziri wa mazingira wa Afrika Kusini , Edna Molewa akihutubia washirikia wa hafla ya siku ya kimataifa ya Nelson Mandela
UN Photo/Rick Bajornas)
Waziri wa mazingira wa Afrika Kusini , Edna Molewa akihutubia washirikia wa hafla ya siku ya kimataifa ya Nelson Mandela

Na Rais wa Baraza Kuu Miroslav Lajczak aliyeendesha hafla nzima ya kumbukizi hiyo akasisitiza ya kuzingatia kutoka kwa Mandela kila tumkumbukapo "Kwanza Nelson Mandela alitufundisha majadiliano, kwamba ghasia na vita vinaturejesha nyuma lakini majadiliano yanaweza kutusongesha mbele, somo la pili ni kuhusu amani, Nelson Mandela anaamini kwamba amani haimanishi tu kutokuwa na vita ni lazima iwe zaidi ya utamaduni ulio ndani ya maisha ya watu sio tu katika kazi zao na naamini kwamba rais Mandela Rais Nelson Mandela alikuwa mmoja wa viongozi wa kwanza duniani kutilia msukumo mizizi ya kuzuka kwa vita.”

Ameongeza kuwa Mandela daima atakumbukwa kwa mengi aliyofanya, kuchagiza, kuhimiza na kuyazingatia kwani yalisaidia na yataendela kuisaidia Dunia kama itayazingatia.