Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasichana wanastahili haki sawa na wavulana katika michezo: Maraam

Wasichana wakicheza mpira
News Arabic
Wasichana wakicheza mpira

Wasichana wanastahili haki sawa na wavulana katika michezo: Maraam

Haki za binadamu

Katika harakati za kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya watoto wa kike, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limeanzisha programu maalum ya mchezo wa mpira wa miguu au  kabumbu katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari  nchini Jordan ili kutoa fursa kwa watoto hao wa kike na wasichana kufanya mazoezi.

Nats….
Huyu ni Maraam mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14, na mkimbizi kutoka Syria, akiwa katika kituo cha michezo kwenye kambi ya Za’atari nchini Jordan kwa zaidi ya miaka 6 sasa.
Nats….
Anasema kwa mwaka wa kwanza hakukuwepo na shule wala vituo vyovyote vya aina hiyo hivi sasa kituo kinafanya kazi na wanaonekana wamevalia jezi nyekundu wengine na vizibao vya manjano.


Sauti ya Mariam 
“Jamii  yetu inadhani kwamba wasichana hawapaswi kucheza kabumbu! Sipendezwi na hilo, sio tu mchezo wa wavulana peke yao, bali pia wasichana.”
 

 
Hatimaye Maraam alikutana na mwalimu  kutoka Jordan ambaye alimuonyesha kituo hiki ambako anaweza kucheza mpira wa miguu.
 
Anasema kwamba taratibu walijenga kiwanja na kuweka magoli na ndipo alipoanza kujifunza jinsi ya kucheza mpira wa miguu pamoja na sheria zake.


Sauti ya Mariam
“Maisha hapa kambini hayatendi haki kwa wasichana wa Syria. Familia  nyingi haziwapi ruhusa ya kuja kwenye michezo au  kwenda shule. Nia yangu kwa wasichana wa Syria ni kwamba wasilazimike kuolewa wakati bado ni wadogo.”


Nats…..


Maraam ambaye ameweza kucheza mpira wa miguu kutokana pia na kuungwa mkono na familia yake anasema..
 
Sauti ya Mariam

“Wasichana wanastahili haki sawa na wavulana. Haki ya kucheza mpira wa miguu, kwenda popote wanakotaka kwenda, kuchagua michezo tofauti wanayoitaka, kwenda shule na kujifunza.”