Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali Syria ni tamu na chungu- OCHA

Khaled, mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10, anaeleza Bwana Lowcock kuhusu jinsi anavyofurahia kwenda shule. Alipoteza makazi na familia yake mwaka mmoja uliopita huko Palmyra. Picha: OCHA

Hali Syria ni tamu na chungu- OCHA

Ziara yangu nchini Syria ni sawa na tamu na chungu kutokana na kile ninachoshuhudia, amesema mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa dharura, OCHA, Mark Lowcock.

Ziara yangu nchini Syria ni sawa na tamu na chungu kutokana na kile ninachoshuhudia, amesema mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa dharura, OCHA, Mark Lowcock.

Bwana Lowcock ambaye ametembelea maeneo mbalimbali nchini Syria, ikiwemo mji wa Homs, amesema ameona uharibifu mkubwa wa majengo uliotokana na vita.

Amesema amekutana na wakimbizi wa ndani kutoka Palmira wakiwemo watoto, wanawake na wengi wakiwa wamekumbwa na kiwewe kutokana na miaka sita ya vita.

(Sauti ya Mark Lowcock)

“Nimezungumza haswa na watumishi wa serikali, baadhi ya wahudumu wa afya, baadhi ya walimu na wanataka kurejea nyumbani ili waendelee na mchango wao wa kujenga jamii bora na kuibuka kutoka kiwewe cha kutisha ambacho wengi wamepitia.”

Hata hivyo kwa upande chanya, Bwana Lowcock amesema amefurahia alichoona,,

(Sauti ya Mark Lowcock)

“Lakini pia nimeshuhudia kazi murua kabisa inayofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na miradi ambayo tunafadhiali kupitia OCHA.”