Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanza tena kurejesha wahamiaji nyumbani kwa hiari kutoka Yemen

Wafanya kazi wa UNHCR wakiwakaribisha wakimbizi katika uwanja wa kijeshi wa Pratica di Mare wakitokea Libya
Picha ya UNHCR/Alessandro Penso
Wafanya kazi wa UNHCR wakiwakaribisha wakimbizi katika uwanja wa kijeshi wa Pratica di Mare wakitokea Libya

IOM yaanza tena kurejesha wahamiaji nyumbani kwa hiari kutoka Yemen

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM limeanza tena kazi ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Ethiopia waliosaka hifadhi Yemen.

Akizungumuza na wandishi habari mjini Geneva Uswisi hii leo, msemaji wa IOM, Joel Millman amesema kazi hiyo imeanza tena baada ya kusitisha kwa muda kutokana na hali ya usalama kutoka nzuri nchini Yemen.

Amesema walifanya uchunguzi wa kina wa njia salama ya kusafirisha kwa hiyari wahamiaji hao akisema.

SAUTI YA JOEL MILLMAN

 “ Waethiopia 53 ambao ni wahamiaji walisafirishwa kutoka Yemen. Hilo limetokea jana Julai 12 kwa kutumia utaalamu wa IOM ambapo walipata ushoroba salama na kukodisha meli ili kuondoa wahamiaji kutoka bandari ya  Hodeidah baada ya kupewa kibali maalum na kusafirisha wahamiaji 53 hadi Djibout ambako watapokelewa na maafisa wa IOM na wataratibu usafiri hadi nyumbani kwao.”

Miongoni mwa wahamiaji hao 53 wa Ethiopia ni wanaume 48 na wavulana watano.

Mnamo Juni 22 mwaka huu IOM  ilitangaza kusitisha kwa muda usiojulikana huduma hiyo ya kurejesha nyumbani kwa hiari wahamiaji waliokuwa wamekwama Hodeidah ikitaja sababu za kiusalama kutokana na mashambulio dhidi ya bandari hiyo muhimu ya Yemen.

IOM inasema mbali na kutoa usafiri kwa wahamiaji wanaotaka kurejea nyumbani lakini pia inawapa msaada mwingine..

SAUTI YA JOEL MILLMAN

“ Kwa ushirikiano na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa, IOM imekuwa  ikiwasaidia wahamiaji kwa kuwapa chakula, usafiri kutokaHodeidah,  msaada wa hduma za kiafya, wa kisaikolojia pamoja na maada wa kifedha.’

Hadi sasa IOM imewasaidia kurejea nyumbani kwa hiari kutoka Hodeidah, zaidi ya wahamiaji 483 wa Ethiopia pamoja na wakimbizi wasomali 1,205 kutoka bandari ya Aden.