Chuja:

Joel Millman

Italian Coastguard/Massimo Sestini

Wahamiaji sasa wamehamia njia ya Hispania

Idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya kupitia baharí ya Mediteranea ikiendelea kupungua, imeelezwa kuwa wahamiaji sasa wanatumia zaidi Hispania kama njia ya kuingia barani humo.

Shirika hilo limesema idadi ya wanaoingia kupitia Hispania imezidi ile ya walioingia kupitia Italia mwishoni mwa wiki likiongeza kuwa zaidi ya asilimia 35 ya wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediteranea wamepitia magharibi mwa bahari hiyo ikiwani mara tatu ya waliosajiliwa kipindi kama hiki mwaka jana.

Sauti
2'13"
Olivia Headon/IOM

Wahamiaji kutoka Ethiopia warejea nyumbani

Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM limeanza tena kazi ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Ethiopia waliosaka hifadhi Yemen.Akizungumuza na wandishi habari mjini Geneva Uswisi hii leo, msemaji wa IOM, Joel Millman amesema kazi hiyo imeanza tena baada ya kusitisha kwa muda kutokana na hali ya usalama kutoka nzuri nchini Yemen.

 

Sauti
1'40"
Olivia Headon/IOM

Lindeni wahamiaji-IOM

Wasiwasi huo umetolewa na  mkuu wa operesheni na masuala ya dharura katika shirika hilo ,Mohammed Abdiker mjini Sana’a Yemen baada ya kushuhudia hali ya wahamiaji.

Msemaji wa IOM,Joel Millman amewaeleza waandishi habari mjini Geneva leo amenukuu Mohamed Adiker aliyosema

(Sauti ya Millman) 

Amesema kuwa  Mwezi Agosti mwaka jana  ulimwengu ulishtushwa  wakati vijana kadhaa, raia wa Ethiopia na Somalia,  waliolazimishwa kujitosa baharini na wasafirishaji haramu karibu na mwambao wa Yemen na baadae kupoteza maisha yao.”.

Sauti
1'45"
Picha: IOM/Video capture

Wahamiaji waendelea kuondoka Libya kwa hiari: IOM

Juhudi za kuwasaidia wahamiaji kutoka Libya hadi nchi walikotoka  zasemekana  kuendelea vizuri umesema leo Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM Joel Millman hadi sasa shirika hilo limesaidi wahamiaji 10,171 kurejea kwao salama kutoka Libya kwa msaada  kutoka Umoja wa Ulaya, Muungano wa Afrika pamoja na serikali ya Libya.